Nafasi za Kazi Watanzania wenye sifa na uzoefu mnaalikwa kuomba nafasi zilizo tangazwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu (UN-OHCHR).
Nafasi zilizotangazwa na Utumishi
- Katibu Mkuu Msaidizi – Haki za Binadamu
- Eneo la kazi: Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR), New York.
- Mwisho wa kutuma maombi: 19 Septemba 2025.
- Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu
- Eneo la kazi: Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR), Geneva – Uswisi.
- Mwisho wa kutuma maombi: 19 Septemba 2025.
Sifa na Ujuzi Unaohitajika kwa Nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi
- Uzoefu wa angalau miaka 20 katika haki za binadamu, mahusiano ya kimataifa au fani zinazohusiana.
- Uzoefu wa kufanya kazi kwenye taasisi kubwa zenye tamaduni mchanganyiko.
- Ujuzi kwenye kupanga sera, kuchambua siasa, usimamizi wa programu, na uratibu wa shughuli kwenye mfumo wa kimataifa.
- Rekodi nzuri ya uongozi na usimamizi bora.
- Uwezo wa majadiliano na diplomasia.
- Uwezo wa kufanya kazi vizuri na watu wa tamaduni tofauti na kujenga ushirikiano wenye tija ndani na nje ya taasisi.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments