Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji PDF ametangaza ratiba rasmi ya usaili kwa waombaji wa ajira kupitia mfumo wa ajira (ajira.zimamoto.go.tz). Usaili utafanyika kuanzia tarehe 15 – 20 Disemba, 2025 kuanzia saa 1:00 Asubuhi kwa mujibu wa makundi mbalimbali.
Bonyeza hapa kudownload majina ya walioitwa zimamoto 2025 PDF
Unaweza Pitia pia:
Ratiba ya Usaili kwa Kundi la Kidato cha Nne – 15 Disemba 2025
Waombaji wote walioomba kwa elimu ya Kidato cha Nne (Form Four) watafanyiwa usaili:
- Tarehe: 15 Disemba 2025
- Muda: Saa 1:00 Asubuhi
- Eneo: Mikoa waliyoiandika wakati wa kutuma maombi
Ratiba ya Usaili kwa Shahada na Taaluma Mbalimbali – 15–20 Disemba 2025
Usaili kwa waombaji wenye Shahada na taaluma maalumu utafanyika katika:
- Ukumbi: Andengenye – Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Dodoma
- Muda: Saa 1:00 Asubuhi
- Tarehe: 15–20 Disemba 2025
Jedwali la Ratiba ya Usaili kwa Kila Taaluma
| Taaluma / Kundi | Tarehe ya Usaili | Maelezo |
|---|---|---|
| Michezo (Sportsmen) – Kundi A | 15 Disemba 2025 | Kulingana na orodha kwenye kiambatanisho |
| Michezo (Sportsmen) – Kundi B | 16 Disemba 2025 | Kulingana na orodha kwenye kiambatanisho |
| Michezo (Sportsmen) – Kundi C | 17 Disemba 2025 | Kulingana na orodha kwenye kiambatanisho |
| Emergency Medical Technician | 18 Disemba 2025 | Usaili kwa taaluma ya huduma ya dharura |
| Nursing | 18 Disemba 2025 | Wauguzi wote kwa pamoja |
| Diver (Uzamiaji) | 19 Disemba 2025 | Usaili maalum kwa waombaji wa uzamiaji |
| Fire Fighting & Rescue Profession | 20 Disemba 2025 | |
| Avionics | 20 Disemba 2025 | |
| Civil Engineer | 20 Disemba 2025 | |
| Data Scientist | 20 Disemba 2025 | |
| Motor Vehicle Mechanics | 20 Disemba 2025 | |
| Quantity Surveyor | 20 Disemba 2025 | |
| Marine Engineer | 20 Disemba 2025 | |
| Oil & Gas Engineer | 20 Disemba 2025 | |
| Office Management Secretary | 20 Disemba 2025 | |
| ICT Technician | 20 Disemba 2025 | |
| ICT Network Technician | 20 Disemba 2025 | |
| Madereva | 20 Disemba 2025 | Waje na Leseni Daraja E |
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Fika Siku na Tarehe Uliyopewa
Kila mwombaji anatakiwa kufika kwenye kituo cha usaili kulingana na tarehe na ratiba iliyopangwa.
2. Kuja na Vyeti Halisi
Hakikisheni mnakuja na:
- Cheti cha Kidato cha Nne
- Cheti cha Kidato cha Sita (kama kinahusika)
- Vyeti vya taaluma
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA
3. Madereva – Leseni Daraja E
Waombaji wa nafasi ya udereva wanapaswa kuwasilisha leseni halisi ya Daraja E.
4. Gharama za Usafiri na Malazi
Gharama zote za safari, chakula, na malazi zinabebwa na msailiwa mwenyewe.
Orodha ya Majina ya Wasailiwa zimamoto 2025
Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa pamoja na makundi yao inapatikana kupitia tovuti rasmi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji: www.zimamoto.go.tz.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments