Table of Contents
Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Mkurugenzi Mtendaji kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi anawatangazia waombaji kazi wote waliotuma maombi kwamba usaili utafanyika kuanzia 15 Septemba 2025 hadi 18 Septemba 2025. Waombaji watakaofaulu watachaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Fika siku na muda uliopangwa kwa kada husika.
- Vaeni barakoa (mask) na mje na kitambulisho halali (Mkazi, Mpiga Kura, Kazi, Uraia au Pasipoti).
- Wasilisha vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, stashahada/shahada kulingana na sifa za kazi.
- Testimonials, provisional results, statements of results na results slips hazitakubaliwa.
- Wasailiwa watajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NACTE au NECTA.
- Wenye kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma waje na vyeti vya usajili na leseni hai.
- Hakikisha kuchukua namba ya mtihani kupitia akaunti yako mapema.
- Majina yasiyo kwenye tangazo hili hayakukidhi vigezo.
Ratiba ya Usaili
1. Usaili wa Mchujo
Kada | Tarehe | Saa | Mahali |
---|---|---|---|
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II | 17-09-2025 | 07:00 asubuhi | Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko |
Msaidizi Maendeleo ya Jamii Daraja II | 17-09-2025 | 07:00 asubuhi | Shule ya Sekondari Ikungi |
2. Usaili wa Vitendo
Kada | Tarehe | Saa | Mahali |
---|---|---|---|
Dereva Daraja II | 15-09-2025 | 07:00 asubuhi | Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi |
3. Usaili wa Mahojiano
Kada | Tarehe | Saa |
---|---|---|
Dereva Daraja II | 16-09-2025 | 07:00 asubuhi |
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II | 18-09-2025 | 07:00 asubuhi |
Msaidizi Maendeleo ya Jamii Daraja II | 18-09-2025 | 07:00 asubuhi |
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments