Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa Usaili wa Maandalizi ya Ajira Mpya – Agosti 2025 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote kuwa usaili kwa nafasi mbalimbali utafanyika kuanzia tarehe 11 Agosti, 2025 hadi 18 Agosti, 2025. Waombaji wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuzingatia masharti na ratiba ifuatayo.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

  1. Usaili utafanyika kwa siku na mahali yaliyoainishwa kwenye tangazo hili kwa kila kada.
  2. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi (Kitambulisho cha NIDA, mpiga kura, kazi, uraia, leseni ya udereva, au barua ya Serikali ya Mtaa/Kijiji).
  3. Msailiwa afike na vyeti vyake halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha Nne hadi Shahada, kutegemeana na sifa za kazi aliyoomba.
  4. Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na results slips za Form IV na Form VI hazitakubaliwa.
  5. Msailiwa atagharamia chakula, usafiri na malazi kwa kipindi chote cha usaili.
  6. Wasailiwa waliomaliza masomo nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika (NECTA, NACTVET au TCU).
  7. Kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma lazima zije na vyeti halisi vya usajili na leseni za kazi.
  8. Msailiwa mwenye tofauti ya majina katika nyaraka zake, aletee Deed Poll iliyosajiliwa rasmi.
  9. Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanya usaili wake.

Ratiba ya Usaili wa Maandishi – 11 Agosti 2025

Mahali: Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

  • Afisa Ugavi Msaidizi
  • Afisa Ugavi II
  • Mchumi II
  • Msaidizi wa Kumbukumbu
  • Afisa Utumishi II
  • Afisa TEHAMA II
  • Afisa Masoko II
  • Afisa Hesabu II
  • Afisa Hesabu Msaidizi II
  • Mhandisi II
  • Fundi Sanifu II

Ratiba ya Usaili wa Vitendo – 17 Agosti 2025

Mahali: Dar es Salaam

  • Dereva
  • Mhandisi
  • Fundi Sanifu

Ratiba ya Usaili wa Mahojiano

Tarehe: 17 Agosti 2025
Mahali: DUCE – Dar es Salaam

  • Afisa Sheria
  • Afisa Ugavi Msaidizi
  • Afisa Ugavi II
  • Mchumi II
  • Msaidizi wa Kumbukumbu II
  • Mhasibu II
  • Afisa Utumishi II
  • Afisa TEHAMA II
  • Afisa Masoko II
  • Afisa Hesabu II
  • Afisa Hesabu Msaidizi II

Tarehe: 18 Agosti 2025
Mahali: DUCE – Dar es Salaam

  • Dereva II
  • Mhandisi II
  • Fundi Sanifu II

Wito: Wasailiwa wote wanaombwa kujiandaa kikamilifu na kufika kwa wakati kulingana na ratiba. Kukosa kutekeleza masharti kutapelekea kuondolewa kwenye mchakato wa usaili.

Soma zaidi: