Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama (Oral Interview)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia waombaji wa nafasi mbalimbali waliopata nafasi ya kuendelea na usaili wa ana kwa ana (oral interview) kufuatia usaili wa awali uliofanyika kuanzia 19 hadi 25 Julai 2025 katika vituo mbalimbali.

Taarifa Muhimu kwa Wasailiwa

  1. Usaili utaanza tarehe 11 Agosti 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika vituo vilivyooneshwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa.
  2. Wasailiwa walioomba kada za:
    • Afisa Mwandishi Mwendesha Ofisi II
    • Mwandishi Mwendesha Ofisi II
    • Dereva II
      wataanza na usaili wa vitendo (practical) na watakaofaulu wataendelea na usaili wa ana kwa ana siku hiyo hiyo.
  3. Kila msailiwa anapaswa kufika na vyeti halisi vya:
    • Elimu
    • Taaluma
    • Cheti cha kuzaliwa
    • Kitambulisho chenye picha kinachotambulika na Serikali
  4. Msailiwa asiyefika kwa muda uliopangwa au bila nyaraka tajwa hatasailiwa.
  5. Usaili utafanyika kwenye kituo kilichopangwa kwa jina lako.

Maelekezo kwa Waombaji

  • Kama jina lako halipo kwenye orodha, basi hukupata nafasi ya kuendelea na usaili huu wa pili.
  • Tembelea tovuti ya Tume kuona orodha ya majina na vituo vya usaili:
    www.jsc.go.tz

Mawasiliano kwa Maelezo Zaidi:

0734 219 821 au 0738 247 341
maulizo.ajira@jsc.go.tz

Tume ya Utumishi wa Mahakama – Huduma kwa Umma kwa Haki na Usawa

Soma zaidi: