Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa kwenye Usaili TFS 2025 Kamanda wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), anawataarifu waombaji wote walioomba nafasi za ajira za mkataba wa mwaka mmoja (kwa tangazo lenye Kumb. AC.18/88/01B/42 la tarehe 12/08/2025) kuwa usaili utafanyika kuanzia 22/09/2025 hadi 23/09/2025.
Watakaofaulu wataajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Usaili utafanyika tarehe 22 – 23 Septemba 2025 kuanzia saa 01:00 asubuhi.
- Kila msailiwa lazima awe na kitambulisho cha utambulisho (NIDA, kura, leseni, hati ya kusafiria au barua ya serikali ya mtaa).
- Waje na vyeti halisi: cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV/VI, Stashahada au Astashahada kulingana na sifa.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Wasailiwa wahakikishe wanafika kwa muda na sehemu waliyoainishiwa.
- Waombaji ambao majina yao hayajaorodheshwa, watambue hawakukidhi vigezo.
Ratiba ya Usaili – Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
S/N | Mwajiri | Kada | Mchujo | Vitendo | Mahojiano | Mahali |
---|---|---|---|---|---|---|
1 | TFS – Kanda ya Nyanda za Juu Kusini | Dereva III | 22/09/2025 – TIA Mbeya | 22/09/2025 – TIA Mbeya | 23/09/2025 | TFS Ofisi ya Kanda – Mbeya |
2 | TFS – Kanda ya Nyanda za Juu Kusini | Mtunza Kumbukumbu Msaidizi II | 22/09/2025 – TIA Mbeya | – | 23/09/2025 | TFS Ofisi ya Kanda – Mbeya |
3 | TFS – Kanda ya Nyanda za Juu Kusini | Fundi Sanifu II – Mechanical | – | – | 23/09/2025 | TFS Ofisi ya Kanda – Mbeya |
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments