Walioitwa Kwenye Usaili SUA 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usali SUA leo 2025 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) anapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi za muda kupitia programu maalum ya kuendeleza zao la Parachichi nchini (tangazo la tarehe 29/08/2025), kwamba usaili utafanyika tarehe 26/09/2025 katika Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro.

Waombaji watakaofaulu katika usaili huu watapangiwa vituo vya kazi na Menejimenti ya Chuo. Ni waombaji waliokidhi vigezo vya tangazo la awali pekee ndio walioteuliwa kushiriki.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

  1. Usaili utafanyika tarehe 26/09/2025 katika maeneo yaliyopangwa kwa kila kada.
  2. Kila msailiwa anatakiwa kufika na kitambulisho kimojawapo kati ya:
    • Kitambulisho cha Uraia (NIDA)
    • Kitambulisho cha Mkazi
    • Kitambulisho cha Kazi
    • Kitambulisho cha Mpiga Kura
    • Hati ya Kusafiria
  3. Msailiwa afike na vyeti halisi vya taaluma kulingana na sifa (Cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV/VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada n.k).
    • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na result slips (form IV & VI) hazitakubaliwa.
  4. Kila msailiwa atajigharamia gharama za chakula, usafiri na malazi.
  5. Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa.
  6. Waliosoma nje ya Tanzania wafike na vyeti vilivyothibitishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).
  7. Waombaji ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo.
  8. Msailiwa ambaye taaluma yake inahitaji usajili wa Bodi za Kitaaluma, afike na vyeti halisi vya usajili huo.
  9. Hairuhusiwi kuingia na simu au vifaa vya kielektroniki kwenye eneo la usaili.

Ratiba ya Usaili

TareheMuda wa KuripotiMahaliMaelezo
26/09/2025Saa 1:00 AsubuhiKampasi ya Edward Moringe, MorogoroUsaili wa kada zote zilizotangazwa kupitia programu ya Parachichi

MUHIMU: Wasailiwa wote wanashauriwa kufika mapema, wakiwa na nyaraka sahihi na kuzingatia maelekezo yote.

Pakua PDF hapa.

Soma zaidi: