Hili hapa tangazo na orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 01 Septemba, 2025 hadi 04 Septemba, 2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
- Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, au hati za matokeo za kidato cha IV na VI hawatakubalika na hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
- Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
- Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTVET au NECTA).
- Kwa kada ambazo zinahitaji usajili na bodi zao za kitaaluma, waombaji wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili pamoja na leseni halali za kufanyia kazi.
- Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha hati ya kiapo cha kubadili jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
Ratiba ya Usaili NFRA
1. UsaIli wa Maandishi – 01/09/2025
Mahali: Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
Muda: Saa 1:00 Asubuhi
Na. | Kada |
---|---|
1 | Afisa Hesabu II |
2 | Afisa Hesabu Msaidizi II |
3 | Afisa Kilimo Msaidizi II |
4 | Afisa Masoko II |
5 | Afisa TEHAMA II |
6 | Afisa Utumishi II |
7 | Mhandisi II |
8 | Msaidizi wa Kumbukumbu II |
9 | Mchumi II |
10 | Afisa Ugavi II |
11 | Afisa Ugavi Msaidizi II |
12 | Fundi Sanifu II |
2. UsaIli kwa Vitendo
Na. | Kada | Tarehe | Mahali | Muda |
---|---|---|---|---|
1 | Dereva II | 01/09/2025 | VETA – Chang’ombe, Dar es Salaam | Saa 1:00 Asubuhi |
2 | Mwandishi/Mwendesha Ofisi II | 01/09/2025 | Ofisi za NFRA – Chang’ombe, Dar es Salaam | Saa 1:00 Asubuhi |
3 | Fundi Sanifu II | 02/09/2025 | VETA – Chang’ombe, Dar es Salaam | Saa 1:00 Asubuhi |
3. UsaIli wa Mahojiano – 04/09/2025
Mahali: Chuo cha Bandari
Muda: Saa 1:00 Asubuhi
Na. | Kada |
---|---|
1 | Afisa Hesabu II |
2 | Afisa Hesabu Msaidizi II |
3 | Afisa Kilimo Msaidizi II |
4 | Afisa Masoko II |
5 | Afisa Sheria II |
6 | Afisa TEHAMA II |
7 | Afisa Utumishi II |
8 | Dereva II |
9 | Mhandisi II |
10 | Mhasibu II |
11 | Msaidizi wa Kumbukumbu II |
12 | Mwandishi/Mwendesha Ofisi II |
13 | Fundi Sanifu II |
14 | Mchumi II |
15 | Afisa Ugavi II |
16 | Afisa Ugavi Msaidizi I |
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments