Walioitwa Kwenye Usaili Mji Mbulu

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mbulu anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote waliotuma maombi kuwa usaili utafanyika kuanzia 09 Septemba 2025 hadi 12 Septemba 2025. Waombaji watakaofaulu watachaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

  1. Kila msailiwa ahakikishe anafika siku na muda uliopangwa kwa kada husika.
  2. Wajitahidi kuvaa barakoa (mask) na kuwa na kitambulisho halali (Mkazi, Mpiga Kura, Kazi, Uraia, au Pasipoti).
  3. Waje na vyeti halisi (cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, stashahada/shahada kulingana na sifa za kazi).
  4. Testimonials, provisional results, statements of results na results slips hazitakubaliwa.
  5. Kwa kada ya Dereva II, wahakikishe wanaleta leseni Daraja E/C pamoja na vyeti vya mafunzo ya udereva. Bila hivyo hawataruhusiwa kufanya usaili.
  6. Wasailiwa watajigharamia chakula, usafiri na malazi.
  7. Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NACTE, NECTA).
  8. Wenye majina yanayohitaji usajili wa kitaaluma waje na vyeti halisi vya usajili na leseni hai.
  9. Hakikisha kuchukua namba ya mtihani kupitia akaunti yako mapema.
  10. Hali ya hewa ya Mbulu ni baridi – vaeni mavazi yanayostahimili ubaridi.
  11. Majina yasiyo katika tangazo hili hayakukidhi vigezo.

Ratiba ya Usaili Mbulu

1. Usaili wa Mchujo

MwajiriKadaTareheSaaMahali
Halmashauri ya Mji MbuluMsaidizi wa Kumbukumbu Daraja II11-09-202501:00 asubuhiUkumbi wa Maendeleo ya Jamii (Community Centre)

2. Usaili wa Vitendo

MwajiriKadaTareheMahali
Halmashauri ya Mji MbuluDereva Daraja II09-09-2025Ukumbi wa Maendeleo ya Jamii (Community Centre)
Halmashauri ya Mji MbuluMwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II09-09-2025Ukumbi wa Maendeleo ya Jamii (Community Centre)

3. Usaili wa Mahojiano

MwajiriKadaTareheMahali
Halmashauri ya Mji MbuluDereva Daraja II10-09-2025Ukumbi wa Maendeleo ya Jamii (Community Centre)
Halmashauri ya Mji MbuluMwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II10-09-2025Ukumbi wa Maendeleo ya Jamii (Community Centre)
Halmashauri ya Mji MbuluMsaidizi wa Kumbukumbu Daraja II12-09-2025Ukumbi wa Maendeleo ya Jamii (Community Centre)

Pakua PDF ya majina hapa.

Soma zaidi: