Table of Contents
Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili afya, walimu na kada zingine Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 16/12/2025 hadi 22/12/2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo
Maelezo kwa wasailiwa
- Fika siku ya usaili ukiwa na barakoa na kitambulisho halali (NIDA, kura, uraia, kazi, leseni ya udereva, pasipoti au barua ya serikali ya mtaa/kijiji).
- Leta vyeti halisi (kuzaliwa, elimu – Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Shahada n.k.) kulingana na sifa ya kada uliyoiomba.
- Testimonials, provisional results, statement of results na result slips za Kidato cha IV & VI hazitakubaliwa.
- Gharama za chakula, usafiri na malazi ni za msailiwa mwenyewe.
- Waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NACTVET au NECTA.
- Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, leta vyeti halisi vya usajili na leseni ya kazi.
- Ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal ili kunakili namba ya mtihani kabla ya siku ya usaili.
- Wenye majina yanayotofautiana kwenye nyaraka wawasilishe Deed Poll iliyosajiliwa.
Kwa wanafunzi
- Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026 TAMISEMI
- Form One Selection 2026 TAMISEMI
- Matokeo ya Form Two 2025
- Matokeo ya Kidato cha Pili 2025
RATIBA YA USAILI (Mahojiano)
| MWAJIRI | KADA | TAREHE YA USAILI | MAHALI |
|---|---|---|---|
| MDAs & LGAs | Afisa Muuguzi Msaidizi II (Assistant Nursing Officer Grade II) | 2025-12-16 07:00 | Usa ili katika mikoa yote ya Tanzania Bara na vituo maalum vya Unguja & Pemba kulingana na makazi ya msailiwa |
| MDAs & LGAs | Mfamasia Daraja la II (Pharmacist Grade II) | 2025-12-17 07:00 | Kwenye mikoa yote + vituo maalum Unguja & Pemba (kwa mujibu wa makazi ya msailiwa) |
| MDAs & LGAs | Daktari Daraja la II (Medical Officer Grade II) | 2025-12-17 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Afisa Muuguzi Daraja la II (Nursing Officer Grade II) | 2025-12-17 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Fundi Sanifu Vifaa Tiba Daraja la II (Biomedical Engineering Technician II) | 2025-12-17 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II (Biomedical Engineer II) | 2025-12-17 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja la II (Dental Therapist II) | 2025-12-18 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III C – Somo la Afya ya Wanyama na Uzalishaji | 2025-12-18 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Fiziotherapia Daraja la II (Physiotherapist II) | 2025-12-18 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Afisa Afya Mazingira Daraja la II (Environment Health Officer II) | 2025-12-18 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Msaidizi Afya ya Mazingira II (Environmental Health Assistant II) | 2025-12-18 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Tabibu Daraja la II (Clinical Officer II) | 2025-12-19 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II (Assistant Environmental Health Officer II) | 2025-12-22 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Dobi Daraja la II (Launderer II) | 2025-12-22 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Daktari wa Upasuaji wa Kinywa na Meno II (Dental Surgeon II) | 2025-12-22 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II (Occupational Therapist II) | 2025-12-22 07:00 | Kama ilivyo juu |
| MDAs & LGAs | Msaidizi wa Afya Daraja la I (Health Assistant I) | 2025-12-22 07:00 | Kama ilivyo juu |
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments