Walioitwa kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ametangaza ratiba rasmi ya usaili kwa waombaji wa ajira kupitia mfumo wa ajira (ajira.zimamoto.go.tz). Usaili utafanyika kuanzia tarehe 15 – 20 Disemba, 2025 kuanzia saa 1:00 Asubuhi kwa mujibu wa makundi mbalimbali.

Bonyeza hapa kudownload majina ya walioitwa zimamoto 2025 PDF

Pitia pia:

Ratiba ya Usaili kwa Kundi la Kidato cha Nne – 15 Disemba 2025

Waombaji wote walioomba kwa elimu ya Kidato cha Nne (Form Four) watafanyiwa usaili:

  • Tarehe: 15 Disemba 2025
  • Muda: Saa 1:00 Asubuhi
  • Eneo: Mikoa waliyoiandika wakati wa kutuma maombi

Ratiba ya Usaili kwa Shahada na Taaluma Mbalimbali – 15–20 Disemba 2025

Usaili kwa waombaji wenye Shahada na taaluma maalumu utafanyika katika:

  • Ukumbi: Andengenye – Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Dodoma
  • Muda: Saa 1:00 Asubuhi
  • Tarehe: 15–20 Disemba 2025

Jedwali la Ratiba ya Usaili kwa Kila Taaluma

Taaluma / KundiTarehe ya UsailiMaelezo
Michezo (Sportsmen) – Kundi A15 Disemba 2025Kulingana na orodha kwenye kiambatanisho
Michezo (Sportsmen) – Kundi B16 Disemba 2025Kulingana na orodha kwenye kiambatanisho
Michezo (Sportsmen) – Kundi C17 Disemba 2025Kulingana na orodha kwenye kiambatanisho
Emergency Medical Technician18 Disemba 2025Usaili kwa taaluma ya huduma ya dharura
Nursing18 Disemba 2025Wauguzi wote kwa pamoja
Diver (Uzamiaji)19 Disemba 2025Usaili maalum kwa waombaji wa uzamiaji
Fire Fighting & Rescue Profession20 Disemba 2025
Avionics20 Disemba 2025
Civil Engineer20 Disemba 2025
Data Scientist20 Disemba 2025
Motor Vehicle Mechanics20 Disemba 2025
Quantity Surveyor20 Disemba 2025
Marine Engineer20 Disemba 2025
Oil & Gas Engineer20 Disemba 2025
Office Management Secretary20 Disemba 2025
ICT Technician20 Disemba 2025
ICT Network Technician20 Disemba 2025
Madereva20 Disemba 2025Waje na Leseni Daraja E

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Fika Siku na Tarehe Uliyopewa

Kila mwombaji anatakiwa kufika kwenye kituo cha usaili kulingana na tarehe na ratiba iliyopangwa.

2. Kuja na Vyeti Halisi

Hakikisheni mnakuja na:

  • Cheti cha Kidato cha Nne
  • Cheti cha Kidato cha Sita (kama kinahusika)
  • Vyeti vya taaluma
  • Cheti cha kuzaliwa
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA

3. Madereva – Leseni Daraja E

Waombaji wa nafasi ya udereva wanapaswa kuwasilisha leseni halisi ya Daraja E.

4. Gharama za Usafiri na Malazi

Gharama zote za safari, chakula, na malazi zinabebwa na msailiwa mwenyewe.

Orodha ya Majina ya Wasailiwa 2025

Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa pamoja na makundi yao inapatikana kupitia tovuti rasmi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji: www.zimamoto.go.tz.

Soma zaidi: