Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (MU) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote kuwa usaili wa nafasi mbalimbali za ajira utafanyika kuanzia tarehe 01 Septemba 2025 hadi 02 Septemba 2025.
Waombaji kazi watakaofaulu usaili huu watapangiwa vituo vya kazi kulingana na taratibu za chuo.
Kuitwa kwenye usaili na Maelezo
- Usaili utafanyika kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kwa kila kada (tarehe, muda na mahali pa usaili).
- Kila msailiwa anatakiwa kuvaa barakoa (mask) wakati wa usaili.
- Kila msailiwa lazima awe na kitambulisho cha utambulisho. Vitambulisho vinavyokubalika ni:
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya kusafiria
- Kila msailiwa anatakiwa kuja na vyeti halisi kuanzia:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Cheti cha Kidato cha IV na VI
- Stashahada / Stashahada ya Juu
- Shahada na kuendelea (kulingana na nafasi aliyoomba)
- Haitakubalika kuwasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, Form V/VI Results Slips.
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania lazima wawe na vyeti vilivyohakikiwa na kuidhinishwa na TCU, NACTE au NECTA.
- Waombaji kazi ambao majina yao hayamo kwenye tangazo hili, hawakukidhi vigezo vilivyoainishwa. Wanahimizwa kuomba tena mara nafasi zitakapotangazwa.
- Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuja na vyeti halisi vya usajili na leseni za kazi.
- Wasailiwa wote wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kabla ya siku ya usaili, kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
MUHIMU: Wasailiwa wote wanashauriwa kuzingatia maelekezo haya kikamilifu ili kuepuka kuondolewa kwenye mchakato wa usaili.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments