Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) anapenda kuwarifu waombaji wa nafasi za muda kupitia programu maalum ya kuendeleza zao la Korosho (tangazo la tarehe 29/07/2025) kuwa usaili wa nafasi hizo utafanyika tarehe 23/08/2025 katika Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro.
Waombaji waliokidhi vigezo pekee ndio wameitwa kwenye usaili.
Maelekezo kwa Wasailiwa
- Usaili utafanyika tarehe 23/08/2025 katika muda na sehemu zilizopangwa.
- Fika na kitambulisho halali (Uraia, Kazi, Mpiga Kura, Mkazi au Hati ya Kusafiria).
- Fika na Vyeti halisi vya elimu (Kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada n.k.) kulingana na sifa ulizoomba.
- Testimonials, provisional results, statements of results na slips hazitakubalika.
- Msailiwa atajigharamia usafiri, chakula na malazi.
- Wasailiwa waliomaliza nje ya Tanzania walete vyeti vya TCU, NACTVET au NECTA vilivyohakikiwa.
- Taaluma zinazohitaji usajili wa bodi za kitaaluma ziwasilishwe vyeti halisi vya usajili.
- Simu na vifaa vya kielektroniki haviruhusiwi kwenye eneo la usaili.
- Majina yasiyo kwenye tangazo hili hayakukidhi vigezo. Waombaji wasisite kuomba tena nafasi zitakapotangazwa.
Ratiba ya Usaili
Mwajiri | Nafasi | Idadi | Tarehe | Muda | Mahali |
---|---|---|---|---|---|
Bodi ya Korosho | Afisa Kilimo | 10 | 23/08/2025 | 08:00 Asbh | Dr. Samia Suluhu Hassan Teaching Complex – Edward Moringe Campus, Morogoro |
Bodi ya Korosho | Afisa Kilimo Msaidizi | 40 | 23/08/2025 | 08:00 Asbh | Dr. Samia Suluhu Hassan Teaching Complex – Edward Moringe Campus, Morogoro |
Kumbuka: Waombaji watakaofaulu usaili watapangiwa vituo vya kazi na Menejimenti ya SUA.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments