Walioitwa Kazini Utumishi Sekretarieti ya Ajira

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kazini Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatangazia waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya 04 Januari 2025 na 10 Juni 2025 kuwa majina ya waliofaulu yameorodheshwa kwenye tangazo hili.

Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Maelekezo kwa Waliofaulu

  1. Barua za kupangiwa vituo vya kazi zitapatikana kupitia Akaunti za Ajira Portal kwenye sehemu ya My Applications.
  2. Waombaji wapakue (Download) na wachapishe (Print) barua hizo kisha wazipeleke wanaporipoti kwenye kituo cha kazi kilichoainishwa.
  3. Kuripoti kwa Mwajiri ndani ya muda uliotajwa kwenye barua ya kupangiwa kituo cha kazi.
  4. Wapeleke Vyeti Halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua ya ajira rasmi.

Taarifa kwa Wasiofaulu

  • Wale ambao majina yao hayapo kwenye orodha hii watambue kuwa hawakufaulu usaili/hawakupata nafasi.
  • Wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi zitakapotangazwa tena.
  • Walio na majina yasiyoonekana kwenye orodha watambue kuwa hawakupata nafasi. Pia, tangazo hili linapatikana katika tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira Tanzania https://www.ajira.go.tz/
AinaTareheDownload link
Kuitwa kazini Utumishi12-08-2025Download 1
12-08-2025Download 2
12-08-2025Download 3
Walioitwa kazini Utumishi11-08-2025Download1
11-08-2025Download2

Soma zaidi: