Hili hapa tangazo la orodha ya majina ya walioitwa kazini Naibu Rasi – Mipango, Fedha na Utawala wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) anapenda kuwataarifu waombaji kazi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 27 Julai, 2025 kuwa matokeo ya usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kukamilisha taratibu mbalimbali za ajira kuanzia tarehe 28 Agosti, 2025 hadi 11 Septemba, 2025 kwa kufika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE).
Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)
Tarehe na Matokeo ya Usaili
- Usaili ulifanyika: 27 Julai, 2025
- Waombaji waliofaulu wanatakiwa kukamilisha taratibu za ajira kuanzia:
28 Agosti, 2025 – 11 Septemba, 2025
Mahali pa Kuripoti
- Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)
- Kuanzia saa 2:00 asubuhi
Nyaraka Muhimu za Kuwasilisha
Waombaji waliofaulu wanatakiwa kuwasilisha kwa ajili ya uhakiki:
- Vyeti halisi vya masomo kuanzia Kidato cha IV na kuendelea, pamoja na nakala zilizoidhinishwa na Wakili/Hakimu.
- Cheti cha kuzaliwa.
- Nakala au namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Picha ndogo tatu za rangi (passport size).
Kwa Waombaji Wasiofaulu
- Wale majina yao hayajatajwa katika tangazo hili, wametambuliwa hawakufaulu/hawakupata nafasi.
- Wanahimizwa kuomba tena pale nafasi mpya zitakapokuwa zimetangazwa.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments