Hii hapa orodha ya majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Chuo cha Arusha Technical College (ATC) 2025/2026 Orodha hii inajumuisha waombaji wa kozi mbalimbali za Diploma na Shahada za Ufundi, kulingana na vigezo vilivyowekwa na TCU pamoja na chuo chenyewe.
Wanafunzi waliopata nafasi hii wanatakiwa kuthibitisha udahili wao kupitia mfumo wa TCU na kufuata taratibu zote za usajili kama zilivyoelekezwa na chuo.
Arusha Technical College (ATC)
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) ni taasisi ya elimu ya juu iliyopo mkoani Arusha, Tanzania. Chuo hiki kinatambulika kwa kutoa mafunzo ya vitendo na nadharia katika fani mbalimbali za ufundi kama uhandisi, ICT, ujenzi, umeme, mitambo na sayansi ya nishati. ATC kimekuwa ni chuo kinachoandaa wataalamu wenye ujuzi mkubwa wa kutatua changamoto za kitaalamu na kiufundi nchini na nje ya nchi.
Jinsi ya Kuangalia Waliochaguliwa
Wanafunzi wanaotaka kuthibitisha kama wameteuliwa kujiunga ATC wanaweza:
Au Pakua orodha ya waliochaguliwa kujiunga na ATC hapa
- Kutembelea tovuti rasmi ya ATC www.atc.ac.tz.
- Kupitia tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz) ambapo majina ya waliochaguliwa huchapishwa.
- Kupakua orodha ya waliochaguliwa iliyowekwa kwenye matangazo ya chuo.
Fomu za Kujiunga na Taratibu
Baada ya kuthibitishwa, kila mwanafunzi anatakiwa:
- Kupakua fomu za kujiunga (Joining Instructions) kupitia tovuti ya chuo.
- Kusoma maelekezo yote kuhusu ada, makazi na vifaa vinavyohitajika.
- Kuhakikisha anathibitisha udahili wake kupitia mfumo wa TCU ndani ya muda uliopangwa.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
- Wanafunzi wote lazima wakamilishe usajili mapema kabla ya kufungua kwa muhula.
- Malipo ya ada na gharama zingine yanafanyika kupitia akaunti maalum zilizotolewa na chuo.
- Ni muhimu kuhifadhi nakala za nyaraka zote muhimu (vyeti, picha na vitambulisho).
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments