Ufadhili wa Masomo NACTVET kwa Diploma

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST), linapenda kutangaza ufadhili kamili wa masomo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria. Masomo haya ni ya Cheti cha Juu (BTS – NTA Level 7) katika fani za mafunzo ya ufundi.

Sifa za Mwombaji:

  1. Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE/Form IV)
  2. Awe na Stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma) ya fani husika yenye GPA ya angalau 3.5 kutoka taasisi inayotambulika
  3. Aliyesoma nje ya nchi lazima apate uthibitisho wa usawa wa vyeti kutoka NECTA, NACTVET au TCU
  4. Vyeti vya taaluma vitafsiriwe kwa Kifaransa au Kiarabu na kuthibitishwa (huduma ya tafsiri: Baraza la Kiswahili 0754566548)
  5. Umri usiozidi miaka 30
  6. Awe na uthibitisho wa umahiri wa lugha ya Kiingereza au Kifaransa kutoka taasisi inayotambulika
  7. Awe na pasipoti halali
  8. Awe na cheti cha kuzaliwa
  9. Awe na ripoti ya afya ya karibuni ikithibitisha hana magonjwa ya kuambukiza na yuko katika hali nzuri kiafya

Masharti ya Ufadhili

  • Serikali ya Algeria itagharamia kila kitu isipokuwa nauli ya ndege.
  • Mwombaji atapaswa kununua tiketi ya kwenda na kurudi Algeria kwa gharama zake.

Jinsi ya Kuomba

  • Pakua fomu ya maombi kupitia tovuti:
    www.nactvet.go.tz
  • Mwisho wa kutuma maombi: 10 Agosti 2025

Utumaji wa Maombi

a) Nakala ya kielektroniki (softcopy) tuma kwa:
info@nactvet.go.tz na nakala kwa: dora.tesha@nactvet.go.tz

b) Nakala ya kawaida (hardcopy) peleka au tuma kwa:
Katibu Mtendaji,
NACTVET,
Jiji la Serikali Mtumba,
City Commercial Complex – Ghorofa ya 1,
Mtaa wa Madukani, S.L.P. 387,
DODOMA

Angalizo:
Serikali ya Tanzania haitatoa mkopo wala msaada wa kifedha kwa waombaji wa ufadhili huu.

Kwa maelezo zaidi:
0759 435 779 au 0735 442 980

Soma zaidi: