Table of Contents
Hili hapa tangazo la Ufadhili wa Kujiendeleza Watumishi Kada za Afya 2025 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anawatangazia watumishi wote wa Serikali waliopata udahili wa kusoma masomo ya Shahada ya Uzamili (Postgraduate) katika fani za afya kwa mwaka wa masomo 2025/2026, kwamba ufadhili wa Samia Health Super Specialization Program 2025 umefunguliwa.
- Kipindi cha kuwasilisha maombi: kuanzia 20/08/2025 hadi 12/09/2025.
- Maombi yatawasilishwa kwa njia ya kielektroniki pekee kupitia link iliyotolewa na Wizara.
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo hayatafanyiwa kazi.
Manufaa ya Ufadhili
- Kwa vyuo vya nje ya nchi: Ada ya masomo, posho ya kujikimu, nauli na posho ya utafiti.
- Kwa vyuo vya ndani ya nchi: Ada ya masomo na posho ya utafiti (wakati wa kipindi cha utafiti).
Vigezo vya Jumla vya Mwombaji
- Kuwasilisha maombi rasmi kupitia Post-graduate Sponsorship Online Application System.
- Awe Raia wa Tanzania na Mtumishi wa Serikali.
- Awe na barua ya udahili (admission letter) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali (ndani au nje ya nchi).
- Awe anakwenda kusoma masomo ya Ubingwa (Specialization) au Ubingwa Bobezi (Super-specialization).
- Kwa wanaoomba kusoma nje ya nchi: Taaluma hiyo isiwe inapatikana ndani ya nchi.
- Awe na uzoefu wa angalau miaka 3 kazini (ambatanisha barua ya ajira na uthibitisho wa kudumu kazini).
- Ufadhili utazingatia uhaba wa taaluma katika kituo cha kazi cha mwombaji.
Vipaumbele vya Ufadhili
- Wataalamu waliopendekezwa na taasisi zao kwa ajili ya mafunzo ya kimkakati.
- Watumishi wanaotarajiwa kurudi katika vituo vyao au kupangiwa vituo kulingana na uhitaji.
- Waombaji waliodahiliwa katika fani za menejimenti na uendeshaji wa huduma za afya:
- Health Monitoring and Evaluation
- Health Systems Management
- Health Policy and Planning
- Health Economics
- Health Financing
- Health Promotion
- Health Laws
- Waombaji waliodahiliwa katika fani za kipaumbele za kibingwa.
Maeneo ya Kipaumbele
- Ngazi ya Afya ya Msingi:
- Obstetric and Gynecology
- Pediatrics and Child Health
- Internal Medicine
- General Surgery
- Ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa na Kanda:
- Obstetric and Gynecology
- Pediatrics and Child Health
- Internal Medicine
- Emergency Medicine
- General Surgery
- Orthopedic Surgery
- Anaesthesiology
- Radiology
- Taaluma nyingine za kibingwa kulingana na kada husika.
Hii ni nafasi muhimu ya kuboresha uwezo wa kitaaluma wa watumishi wa afya kwa manufaa ya taifa.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments