Ratiba ya Upimaji wa Taifa wa Darasa la Pili 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hii hapa Ratiba ya Upimaji wa Taifa wa Darasa la Pili 2025 Novemba 2025 NECTA ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa Sheria mwaka 1973 yenye jukumu la kusimamia mitihani ya kitaifa nchini Tanzania. Kabla ya mwaka 1973, mitihani yote ya kitaifa ilisambimiwa na Kitengo cha Mitaala na Mitihani cha Wizara ya Elimu baada ya Tanzania Bara kujitoa kwenye Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki mwaka 1971.

Baada ya kuanzishwa, NECTA ilichukua jukumu hilo, lakini masuala ya mitaala yaliendelea kusimamiwa na Wizara ya Elimu pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi kuanzishwa kwa taasisi huru nyingine, Taasis ya Maendeleo ya Mitaala (ICD), mwaka 1975, ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Taasis ya Elimu Tanzania (TIE) mwaka 1993.

Ratiba ya Upimaji

TareheSikuMuda (Saa)Namba MfichoStadi
18.11.2025Jumanne2:00 – 2:40R02 / R02EKuandika: Basic English Language Skills (Writing)
2:40 – 3:40—Mapumziko
3:40 – 4:30R03 / R03EStadi ya Kuhesabu (Arithmetic Skills)
19.11.2025Jumatano2:00 – 5:00R01Stadi ya Kusoma
20.11.2025Alhamisi——Shule zilizo na wanafunzi zaidi ya 300: Upimaji wa Stadi ya Kusoma unaendelea

Pakua hapa PDF ya ratiba.

Maelekezo kwa Wakuu wa Shule

  1. Hakikisha una ratiba ya upimaji ya mwaka 2025 iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
  2. Wanafunzi wote waliosajiliwa lazima washiriki katika upimaji wa Stadi ya Kusoma, Kuandika (Writing: Basic English Language Skills) na Kuhesabu (Arithmetic Skills).
  3. Kila stadi ifanyike kwa tarehe na muda uliopangwa kwenye ratiba hii.
  4. Shule zilizosajili wanafunzi zaidi ya 300 zitaendesha Upimaji wa Stadi ya Kusoma kwa siku mbili: 19.11.2025 na 20.11.2025.
  5. Usimamizi wa upimaji ufanyike kwa kuzingatia Mwongozo wa Upimaji wa Kitaifa wa Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu Darasa la Pili Ngazi ya Shule unaopatikana katika tovuti ya NECTA: www.necta.go.tz.

Soma zaidi: