Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Pili (FTNA) 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Muhtasari wa Maelekezo kwa Wanafunzi – Ratiba ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) 2025

FTNA ni tathmini ya maendeleo inayolenga kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na kutoa mrejesho kwa walimu, wanafunzi na wadau wa elimu ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.

Mambo Muhimu

  1. Kila somo lina examination format inayoeleza muundo wa mtihani na maudhui yatakayopimwa.
  2. Ratiba ya mtihani itaheshimiwa hata ikitokea kwenye siku ya sikukuu ya kitaifa.
  3. Ikitokea tofauti ya taarifa, muda na tarehe iliyo kwenye karatasi ya mtihani ndiyo itakayofuata.

Maelekezo kwa Wanafunzi

  1. Fanya mtihani katika kituo ulichoandikishwa, isipokuwa kama umepewa taarifa rasmi ya kubadilishiwa kituo.
  2. Fuata maagizo ya wasimamizi wa mtihani muda wote.
  3. Fika kwenye chumba cha mtihani kwa muda uliopangwa; ukichelewa zaidi ya dakika 30 baada ya kuanza hutaruhusiwa kuingia.
  4. Ruhusiwa kutoka chumba cha mtihani baada ya dakika 30 za mwanzo kwa ruhusa ya msimamizi.
  5. Leta vifaa vinavyoruhusiwa pekee. Udanganyifu au kusaidia udanganyifu unaweza kusababisha kufutiwa matokeo na kufungiwa kufanya mitihani ya baraza siku zijazo.
  6. Mawasiliano kati ya wanafunzi hayaruhusiwi. Inua mkono kama unahitaji msaada.
  7. Andika namba yako ya mtihani kwenye kila ukurasa wa kijitabu cha majibu. Usitumie jina lako au alama yoyote ya utambulisho.
  8. Ukipatikana na hatia ya udanganyifu unaweza kufutiwa mtihani wote.
  9. Usiharibu wala kutoa vifaa vya mtihani bila ruhusa.
  10. Jibu kwa lugha iliyoelekezwa kwenye mtihani.
  11. Tumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi; michoro ifanywe kwa penseli.
  12. Uvutaji sigara umepigwa marufuku ndani ya chumba cha mtihani.
  13. Kila mwanafunzi lazima afanye mitihani aliyosajiliwa.
  14. Wakati wa maandalizi ya mitihani ya vitendo, wanafunzi wote wasubiri kwenye chumba maalumu kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi mtihani uanze.
  15. Watahiniwa wa kujitegemea lazima walete barua ya utambulisho inayowaruhusu kufanya mtihani; hawaruhusiwi kuandika chochote kwenye barua hiyo.

Pakua PDF hapa ya ratiba

Soma zaidi: