Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili Tume ya Mahakama 2025-26 PDF

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Angalia hapa orodha ya majina walioitwa kwenye usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama 2025-26 PDF inapenda kuwafahamisha waombaji wote wa ajira walioomba nafasi mbalimbali zilizotangazwa tarehe 3 Juni 2025 kuwa, baada ya uchambuzi wa maombi, baadhi ya waombaji wamechaguliwa kushiriki kwenye usaili wa hatua ya kwanza.

Ratiba ya Usaili wa Awali – Julai 2025

Majina ya walioitwa kwenye usaili huo pamoja na tarehe, muda na vituo vya usaili yameorodheshwa katika orodha rasmi iliyowekwa kupitia tovuti ya Tume: www.jsc.go.tz.

Muhimu kufuatwa:

  • Kila msailiwa anafanya usaili katika kituo alichopangiwa tu – hakutakuwa na mabadiliko ya vituo.
  • Usaili huu utafanyika kwa njia ya Kielektroniki (Computer Based Interview).
  • Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na:
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
    • Vyeti halisi vya taaluma (Academic Certificates)
    • Vyeti vya sekondari (O-level/A-level)

Waombaji watakaofaulu hatua ya kwanza, watajulishwa kuhusu hatua inayofuata, ambayo ni usaili wa kujieleza (Oral Interview) na/au Vitendo (Practical Interview) kupitia tovuti ya Tume.

Kwa waombaji ambao hawajaona majina yao, wafahamu kuwa hawakufanikiwa kufuzu kwa hatua ya usaili wa awali.

Ratiba ya Usaili wa Awali Tume ya Mahakama Julai 2025

Na.TareheSikuKada Zilizoitwa
119 Julai 2025JumamosiMsaidizi wa Kumbukumbu
221 Julai 2025JumatatuAfisa Mwongoza Ofisi, Mwandishi, Mkutubi, Msaidizi wa Maktaba
322 Julai 2025JumanneWataalamu wa Ufundi: Umeme, Bomba, Uchoraji, Useremala, Uchomeleaji, Friji
423 Julai 2025JumatanoHakimu Mkazi, Mpishi, Msaidizi wa Hesabu
524 Julai 2025AlhamisiOpereta wa Kompyuta, Opereta Msaidizi, Dereva
625 Julai 2025IjumaaMlinzi, Msaidizi wa Ofisi
726 Julai 2025JumamosiAfisa Utumishi

Maelezo Zaidi na Mawasiliano:
Tembelea tovuti rasmi: www.jsc.go.tz
Simu: 0734 219 821 au 0738 247 341
Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz

Soma zaidi:

Imetolewa na:
Lydia Churi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Tume ya Utumishi wa Mahakama