Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili Tume ya Mahakama 2025 Disemba PDF

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Angalia hapa orodha ya majina walioitwa kwenye usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama 2025 Disemba PDF inapenda kuwafahamisha waombaji wote wa ajira walioomba nafasi mbalimbali zilizotangazwa tarehe 17 Novemba, 2025 kuwa, baada ya uchambuzi wa maombi, baadhi ya waombaji wamechaguliwa kushiriki kwenye usaili wa hatua ya kwanza.

Bonyeza hapa kudownload tangazo kuitwa kwenye usaili Mahakama

Jinsi ya kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2025

Ratiba ya Usaili wa Awali – Disemba 2025

Majina ya walioitwa kwenye usaili huo pamoja na tarehe, muda na vituo vya usaili yameorodheshwa katika orodha rasmi iliyowekwa kupitia tovuti ya Tume: www.jsc.go.tz.

Muhimu kufuatwa:

  • Kila msailiwa anafanya usaili katika kituo alichopangiwa tu – hakutakuwa na mabadiliko ya vituo.
  • Usaili huu utafanyika kwa njia ya Kielektroniki (Computer Based Interview).
  • Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na:
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
    • Vyeti halisi vya taaluma (Academic Certificates)
    • Vyeti vya sekondari (O-level/A-level)

Waombaji watakaofaulu hatua ya kwanza, watajulishwa kuhusu hatua inayofuata, ambayo ni usaili wa kujieleza (Oral Interview) na/au Vitendo (Practical Interview) kupitia tovuti ya Tume.

Kwa waombaji ambao hawajaona majina yao, wafahamu kuwa hawakufanikiwa kufuzu kwa hatua ya usaili wa awali.

Ratiba ya Usaili wa Awali Tume ya Mahakama Disemba 2025

Na.TareheSikuKada
116 Desemba, 2025JumanneAfisa Utumishi II (Rasilimaliwatu)
217 Desemba, 2025JumatanoAfisa Ununuzi II / Afisa Ugavi II / Afisa Ugavi Msaidizi I
318 Desemba, 2025AlhamisiHakimu Mkazi II / Mhasibu II / Msaidizi Wa Ofisi
422 Desemba, 2025JumatatuDereva II / Mlinzi
523 Desemba, 2025JumanneKompyuta Operata II / Mpishi II

Maelezo Zaidi na Mawasiliano:
Tembelea tovuti rasmi: www.jsc.go.tz
Simu: 0734 219 821 au 0738 247 341
Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz

Soma zaidi:

Imetolewa na:
Lydia Churi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Tume ya Utumishi wa Mahakama