Kila mwaka, Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) hutangaza Orodha ya Waliochaguliwa MUHAS 2025-26 PDF kwa programu mbalimbali. Kwa kingereza unaweza sema “muhas selection 2025” Ikiwa unasubiri kuthibitisha kama umechaguliwa, makala hii itakusaidia kujua jinsi ya kuangalia majina, historia fupi ya MUHAS na nini cha kufanya ukiona jina lako.
Angalia hapa katika PDF waliochaguliwa
MUHAS Ni Chuo Gani?
Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) ni moja ya vyuo vikuu vikubwa na vinavyoaminika zaidi Tanzania. Kina makundi mengi ya kozi kuanzia shahada ya kwanza hadi shahada za uzamili na udaktari. Kila mwaka MUHAS hutoa nafasi kwa maelfu ya wanafunzi kutoka kona zote za nchi na nje ya nchi.
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatoa kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Shahada, Diploma, Shahada ya Uzamili na Uzamivu katika nyanja za Afya na Sayansi Shirikishi. Baadhi ya kozi zinazotolewa ni Udaktari wa Binadamu (MD), Udaktari wa Meno (DDS), Uuguzi, Famasia, Sayansi ya Maabara, Afya ya Jamii, Uhandisi wa Tiba, Lishe, Fiziotherapi, Teknolojia ya Mionzi, Utaalamu wa Upasuaji, na Sayansi ya Afya ya Jamii. Pia MUHAS hutoa programu za Uzamili katika fani mbalimbali za tiba, utafiti wa afya, na menejimenti ya huduma za afya.
Jinsi ya Kuangalia Orodha ya Waliochaguliwa MUHAS
Ili kupata orodha ya Waliochaguliwa MUHAS, fuata hatua hizi rahisi:
- Tembelea tovuti rasmi ya MUHAS:Â muhas.ac.tz
- Nenda sehemu ya ‘Admissions’ au ‘Selected Applicants’.
- Chagua mwaka wa udahili unaohusika.
- Pakua faili lenye majina ya waliochaguliwa.
- Tumia namba yako ya usajili au jina lako kutafuta kwa haraka.
Kama umechaguliwa na Tamisemi angalia hapa
Usisahau kuwa na kifaa chenye mtandao mzuri ili kupakua bila usumbufu.
1. Jinsi ya Kuomba Kujiunga MUHAS:
Kuomba kujiunga MUHAS ni rahisi. Wanafunzi wanatakiwa kutuma maombi kupitia mfumo wa udahili mtandao (Online Application System) unaopatikana kwenye tovuti rasmi ya MUHAS (muhas.ac.tz). Unatakiwa kuwa na vyeti sahihi vya masomo na kulipia ada ya maombi kama ilivyoelekezwa.
2. Ada na Gharama:
Ada MUHAS inategemea aina ya kozi na ngazi ya masomo. Kwa kawaida, ada ya shahada ya kwanza huanzia kati ya TZS 1,000,000 hadi TZS 1,500,000 kwa mwaka, bila kujumuisha gharama za malazi na chakula. Wanafunzi wanashauriwa kuwasiliana na ofisi za udahili au kutembelea tovuti ili kupata taarifa za kina na viwango vya ada kwa kila programu.
Nini Cha Kufanya Baada ya Kuthibitishwa MUHAS
Hongera kama jina lako limo kwenye Orodha ya Waliochaguliwa MUHAS! Sasa zingatia mambo haya muhimu:
- Lipa Ada ya Kuthibitisha Nafasi: Hii itahakikisha nafasi yako haipotei.
- Andaa Nyaraka Muhimu: Vyeti vya awali, cheti cha kuzaliwa, picha za passport size na barua muhimu.
- Angalia Tarehe Muhimu: Jua tarehe ya kuripoti na ratiba ya mafunzo ya awali.
- Wasiliana na Ofisi ya Udahili: Kama una swali au shida yoyote, wasiliana mapema na ofisi za udahili MUHAS.
Hitimisho
Waliochaguliwa MUHAS wanapata nafasi ya kusoma katika chuo kikuu bora kinachotoa elimu yenye viwango vya kimataifa. Hakikisha unaandaa kila kitu mapema ili kuanza safari yako ya masomo bila usumbufu.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments