Hii haoa orodha ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na chuo zaidi ya kimoja PDF Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma kuwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 imekamilika. Jumla ya waombaji na nafasi zilikuwa kama ifuatavyo:
Angalia hapa majina ya waliochaguliwa TCU pdf.
Orodha ya Waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo kimoja au Programu zaidi ya moja hii hapa PDF ya majina.
Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo
Kigezo | Takwimu 2025/2026 | Kumbukumbu 2024/2025 | Tofauti |
---|---|---|---|
Idadi ya waombaji | 146,879 | – | – |
Idadi ya vyuo vilivyoruhusiwa | 88 | – | – |
Idadi ya programu | 894 | 856 | +38 |
Nafasi za udahili | 205,652 | 198,986 | +6,666 (3.3%) |
Waombaji waliodahiliwa | 116,596 (79.4%) | – | – |
Waombaji Waliodahiliwa Zaidi ya Chuo Kimoja
Waombaji waliopata nafasi katika zaidi ya chuo kimoja wanapaswa:
- Kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja pekee kati ya tarehe 03 – 21 Septemba 2025.
- Uthibitisho unafanyika kwa kutumia namba ya siri (confirmation code) iliyotumwa kwa SMS au barua pepe.
- Wale ambao hawajapokea ujumbe wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa namba ya uthibitisho.
- Orodha ya majina ya waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja inapatikana katika tovuti ya TCU: www.tcu.go.tz.
Awamu ya Pili ya Udahili
TCU inatangaza kufunguliwa kwa Awamu ya Pili ya Udahili kuanzia 03 – 21 Septemba 2025.
Fursa hii ni kwa:
- Waombaji ambao hawakuwasilisha maombi kwenye Awamu ya Kwanza.
- Waombaji ambao hawakupata nafasi ya kudahiliwa kutokana na ushindani.
Maelekezo:
- Vyuo vya Elimu ya Juu vimetakiwa kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.
- Waombaji wanashauriwa kuzingatia ratiba na taratibu zilizowekwa kwenye kalenda ya udahili kupitia tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).
Wito kwa Waombaji
- Waombaji wanakumbushwa kuwa masuala yote ya udahili au uthibitisho yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.
- Vyuo vimeelekezwa kutoa msaada wa haraka kwa wanafunzi watakaokutana na changamoto za kiufundi.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments