Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa rasmi tarehe 1 Julai, 2008 kupitia Tangazo la Serikali Na. 189 la mwaka huo, chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma (Cap 245 R.E. 2002). Lengo kuu lilikuwa kuboresha utoaji wa huduma kwa umma, kuweka mazingira rafiki kwa usimamizi mzuri wa kazi, na kuboresha ubora wa huduma za ajira ambazo hapo awali zilikuwa chini ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.
Kazi Kuu za TaESA ni pamoja na

- Kuunganisha watu wanaotafuta kazi na fursa zilizopo.
- Kuratibu, kusaidia na kufuatilia ajira za mipakani (cross-border placements).
- Kukusanya, kuchambua na kusambaza taarifa kuhusu soko la ajira kwa wadau na umma kwa ujumla.
- Kutoa mafunzo ya mbinu za kutafuta kazi, ushauri wa kazi na mwelekeo wa kitaaluma.
- Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusu huduma za ajira.
Ofisi za TaESA kwa sasa zinapatikana Dar es Salaam na Mwanza
- Dar es Salaam: Tupo kwenye Barabara ya Bibi Titi Mohamed/Morogoro, karibu kabisa na jengo la Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA).
- Mwanza: Ofisi zetu zipo karibu na makutano ya Barabara ya Stesheni ya Reli na Kenyatta, mkabala na Lake Hotel.
Namba za TAESA na Ofizi zilipo.
1. Makao Makuu – Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu
Tanzania Employment Services Agency
S.L.P 80348,
Dar es Salaam
Simu: 0735 221022 / 0739 221022
Barua pepe: info@taesa.go.tz
2. Kanda ya Ziwa – Mwanza
Msimamizi wa Kanda
Tanzania Employment Services Agency
S.L.P 1192, Mwanza
Simu: +255 28 2541840/1
Barua pepe: mwanza@taesa.go.tz
3. Kanda ya Kaskazini – Arusha
Msimamizi wa Kanda
Tanzania Employment Services Agency
S.L.P 12552, Arusha
Simu: 0736 551055
Barua pepe: arusha@taesa.go.tz
4. Kanda ya Mashariki na Pwani – Dar es Salaam
Msimamizi wa Kanda
Tanzania Employment Services Agency
S.L.P 80343, Dar es Salaam
Simu: 0735 221022 / 0739 221022
Barua pepe: daresalaam@taesa.go.tz
5. Kanda ya Kati – Dodoma
Msimamizi wa Kanda
Tanzania Employment Services Agency
S.L.P 114, Dodoma
Simu: 0735 551055
Barua pepe: dodoma@taesa.go.tz
Maelezo muhimu kuhusu mfumo wa TaESA na namna ya kuutumia, fata linki hizo hapo chini;
- Kufungua Account pitia hapa
- Kujisajili TAESA
- Kuingia katika akaunti yako ya taesa
- Jinsi ya kutumia mfumo wa TAESA
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments