Hili hapa tangazo na orodha ya majina ya nyongeza walioitwa kwenye usaili Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 01-09-2025 hadi 02-09-2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Vaa barakoa siku ya usaili.
- Kuwa na kitambulisho halali (uraia, mpiga kura, mkazi, kazi au pasipoti).
- Leta vyeti halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV na kuendelea.
- Testimonials, provisional results, statements of results na slips hazitakubaliwa.
- Gharamia chakula, usafiri na malazi binafsi.
- Vyeti vya nje ya nchi vihakikiwe na TCU, NACTE au NECTA.
- Kada zinazohitaji usajili waje na vyeti na leseni halisi.
- Namba za mtihani zinapatikana kwenye akaunti binafsi za waombaji.
- Waliokosa majina kwenye tangazo hili hawakukidhi vigezo.
Ratiba ya Usaili
1. Usaili wa Mchujo – 01/09/2025
Mwajiri | Kada | Tarehe | Muda | Mahali |
---|---|---|---|---|
Chuo Kikuu Mzumbe (MU) | Tutorial Assistant (Accounting and Finance) | 01-09-2025 | 07:00 AM | Samora Hall |
Chuo Kikuu Mzumbe (MU) | Tutorial Assistant (Linguistics in Kiswahili) | 01-09-2025 | 07:00 AM | Samora Hall |
2. Usaili wa Mahojiano – 02/09/2025
Mwajiri | Kada | Tarehe | Muda | Mahali |
---|---|---|---|---|
Chuo Kikuu Mzumbe (MU) | Tutorial Assistant (Accounting and Finance) | 02-09-2025 | 07:00 AM | SOB Conference Room |
Chuo Kikuu Mzumbe (MU) | Tutorial Assistant (Linguistics in Kiswahili) | 02-09-2025 | 07:00 AM | M&E Class 2 |
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments