Eneo: Ubena Zomozi, Chalinze – Mkoa wa Pwani
Muda: Miezi 5
Idadi ya Nafasi: 2
Muda wa Kuanza: Mara moja
Mwisho wa Kutuma Maombi: 10 Agosti, 2025
Kuhusu Programu:
Mbogo Ranches Company Ltd kwa kushirikiana na timu ya wataalamu wa mifugo ya Mbogo Ranch, inatangaza fursa za mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa fani ya Sayansi ya Mifugo na taaluma zinazohusiana.
Mafunzo haya yatatoa ujuzi wa kina na mafunzo kwa njia ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji na usimamizi wa mifugo.
Unachojifunza:
Wahitimu watafundishwa na kuongozwa na wataalamu wabobezi katika maeneo yafuatayo:
- Ufugaji wa kisasa na usimamizi wa mifugo
- Afya ya wanyama na udhibiti wa magonjwa
- Lishe na mpango wa ulishaji kulingana na aina ya mnyama
- Mbinu za uzalishaji na ulishaji
- Usimamizi wa:
- Mbuzi na kondoo
- Mbuzi wa maziwa
- Ng’ombe
- Farasi
- Kuku na ndege wa kufugwa
- Utunzaji wa kumbukumbu za shamba na taarifa muhimu
- Uzoefu wa moja kwa moja wa kazi kwenye ranchi ya kitaalamu
Sifa za Mwombaji
- Awe na stashada au stashahada ya Animal Science, Veterinary Medicine, Livestock Production, au fani inayohusiana
- Awe na nia kubwa ya kujifunza ufugaji, na utayari wa kufanya kazi maeneo ya vijijini
- Awe na nidhamu, mawasiliano mazuri na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano
- Wahitimu wapya au waliomaliza masomo na kusubiri kuhitimu wanakaribishwa
Faida kwa Washiriki:
- Ujuzi wa kipekee chini ya mazingira halisi ya ranchi
- Nafasi ya kuajiriwa baada ya programu, kulingana na utendaji
- Cheti cha ushiriki na kukamilisha mafunzo
Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma:
- Barua ya maombi yenye kueleza nia yako
- CV (Wasifu)
- Nakala ya cheti au academic transcript (ikiwa ipo)
Tuma kwenda kupitia barua pepe:
applications@aft.co.tz
Mwisho wa kutuma maombi: 10 Agosti, 2025
Ni waombaji waliowekwa kwenye mchujo (shortlisted) watakaowasiliana.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments