Table of Contents
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za kujiunga na Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu katika fani zifuatazo:
- Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali – Miaka 2
- Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi – Miaka 2
- Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu – Miaka 2
- Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Sayansi na Hisabati) – Miaka 3
Mafunzo yatatolewa katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali.
Sifa za Kujiunga
A. Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali/Msingi/Maalumu (Miaka 2)
- Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I–III na Principal Pass mbili (02).
- Waliosoma Economics, Commerce au Book Keeping waombe kozi ya Elimu ya Awali.
- Walimu wenye Cheti cha Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi pia wanaruhusiwa kuomba.
B. Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi – Sayansi & Hisabati (Miaka 3)
- Wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I–III.
- Wenye alama C au zaidi katika masomo matatu, na mawili kati ya haya:
- Basic Mathematics
- Biology
- Chemistry
- Physics
- Information and Computer Studies
- Computer Science
Vyuo na Aina ya Mafunzo
Jedwali la vyuo na kozi husika limeambatanishwa na tangazo hili kwenye tovuti ya Wizara.
Maelekezo ya Maombi
- Maombi yafanywe kwa kuzingatia sifa zilizotajwa.
- Mafunzo yatatolewa na vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali vilivyoteuliwa na Wizara.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments