Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe anatangaza nafasi za kazi zilizotokana na kibali cha ajira kipya chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waombaji wenye sifa wanakaribishwa kuomba nafasi kama zilivyoainishwa hapa chini:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Kada ya Kazi | Idadi ya Nafasi | Sifa za Mwombaji | Ngazi ya Mshahara |
---|---|---|---|
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II | 4 | – Elimu ya Kidato cha IV/VI- Stashahada (Diploma NTA Level 6) ya Masjala kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali- Ujuzi wa kompyuta | TGS C1 |
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II | 5 | – Elimu ya Kidato cha IV/VI- Diploma ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6- Uwezo wa hatimkato maneno 100/min (Kiswahili & Kiingereza)- Ujuzi wa programu za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher) | TGS C1 |
Dereva Daraja II | 13 | – Elimu ya Kidato cha IV/VI- Leseni daraja E au C yenye uzoefu ≥ mwaka 1 bila kusababisha ajali- Cheti cha Basic Driving Course (VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali) | TGS B1 |
Muhudumu wa Boti (Deckhand Auxiliaries) | 1 | – Elimu ya Kidato cha IV- Cheti cha Teknolojia ya Uvuvi (FETA) au Cheti cha Uhudumu wa Meli (DMI) au sifa inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali | TGOS A |
Masharti ya Jumla:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi 45.
- Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo wa maombi.
- Waambatishe wasifu binafsi (CV) yenye mawasiliano na majina ya wadhamini watatu.
- Vyeti vyote vya elimu na taaluma viwe vimeidhinishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Vyeti vya provisional results, statement of results na result slips (Form IV & VI) havikubaliki.
- Waombaji wa kada ya dereva waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Waombaji waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Vyeti vya nje ya nchi viwe vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTVET).
- Taarifa za kughushi hazitakubalika na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira:
https://portal.ajira.go.tz - Pakua PDF ya tangazo hapa
Barua ya maombi ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
S.L.P. 64,
Njombe.
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Septemba, 2025
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments