Table of Contents
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi kumi (10) za kazi baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Nafasi | Majukumu Makuu | Sifa za Mwombaji | Mshahara |
|---|---|---|---|
| Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II (5 Nafasi) | Kuchapa barua/nyaraka za kawaida na za siri. – Kupokea wageni na kuratibu kumbukumbu na ratiba za kazi. | Kidato cha IV/VI. – Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6). – Hatimkato Kiswahili & Kiingereza (100 maneno/dakika). – Ujuzi wa kompyuta (Windows, MS Office, Internet, Email, Publisher). | TGS C |
| Dereva Daraja II (5 Nafasi) | Kukagua gari kabla/baada ya safari. – Kuwapeleka watumishi safari za kikazi na kurekodi safari. | Kidato cha IV. – Leseni Daraja E au C yenye uzoefu ≥ mwaka 1 bila ajali. – Cheti cha mafunzo ya msingi ya udereva (VETA au chuo kinachotambuliwa). | TGS B |
Masharti ya jumla:
- Waombaji wawe raia wa Tanzania, umri kuanzia miaka 18 hadi 45.
- Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu wao.
- Waombaji wa kada ya Dereva II waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Ambatanisha CV, anuani, namba za simu, barua pepe na majina ya wadhamini watatu.
- Ambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na wakili/mwanasheria.
- Testimonials, provisional results, statements of results, na results slips hazitakubaliwa.
- Vyeti vya nje ya nchi vihakikiwe na TCU/NECTA/NACTE.
- Walioacha kazi serikalini hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ni 12 Septemba 2025.
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
https://portal.ajira.go.tz
Barua ya maombi ielekezwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
S.L.P 16,
TARIME.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments