Nafasi za Kazi Wilaya ya Sumbawanga 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga inawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi kumi na tatu (13) za ajira baada ya kupata vibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mwisho wa kutuma maombi: 01 Oktoba 2025
Njia ya kutuma maombi: Kupitia Recruitment Portal https://portal.ajira.go.tz

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

NafasiIdadiMajukumu Makuu (2)Sifa za MwombajiMshahara
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II3– Kuchapa nyaraka za kawaida na siri – Kupokea wageni na kusikiliza shida zaoKidato cha IV/VI, Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6), ufaulu wa Hatimkato (100 maneno/dakika), mafunzo ya Kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, n.k.)TGS C – 1
Dereva Daraja II8– Kukagua gari kabla/baada ya safari – Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikaziKidato cha IV/VI, Leseni ya Daraja C au E, Cheti cha Udereva kutoka VETA/Chuo kinachotambuliwa na Serikali, uzoefu angalau mwaka 1 bila ajaliTGS B – 1
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II2– Kuorodhesha barua zinazoingia/zinazotoka – Kusambaza na kurudisha majaladaKidato cha IV/VI, Stashahada ya Utunzaji wa Kumbukumbu (NTA Level 6), ujuzi wa kutumia kompyutaTGS C – 1

Masharti ya Jumla

  1. Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri miaka 18–45.
  2. Waambatishe cheti cha kuzaliwa, CV yenye anuani, simu na wadhamini 3.
  3. Vyeti vya taaluma lazima viwe vimethibitishwa na Mwanasheria.
  4. Vyeti vya provisional, statement of results na result slips HAVITAKUBALIWA.
  5. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA/NACTVET/TCU.
  6. Waombaji wa kazi ya Dereva lazima waambatishe vyeti vya udereva vinavyoonesha sifa za kupata daraja husika.
  7. Waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  8. Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia Recruitment Portal.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
https://portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi ielekezwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga,
S.L.P 229
SUMBAWANGA

Soma zaidi: