Nafasi za Kazi Wilaya ya Songwe

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Wilaya ya Songwe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na.FA.97/228/01/A/25 ya tarehe 29/04/2025. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo: –

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

1. Dereva Daraja la II – Nafasi 4

Sifa za Mwombaji:

  • Awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
  • Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
  • Awe na leseni ya daraja E au C aliyofanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali
  • Awe amehitimu mafunzo ya msingi ya udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali

Majukumu ya Kazi:

  1. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha usalama
  2. Kuwasafirisha watumishi katika safari za kikazi
  3. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari

Ngazi ya Mshahara:

Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali – TGS B

Maelekezo kwa Waombaji:

  • Maombi yaambatane na barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa na vyeti vifuatavyo:
    • Cheti cha kuzaliwa
    • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
    • Leseni ya udereva ya daraja E au C
    • Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa
    • Wasifu binafsi (CV) unaoonesha anuani ya sasa, namba ya simu na barua pepe
    • Majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE, au TCU)
  • Maombi yasiyoambatishwa na vyeti halisi yaliyoidhinishwa na wakili hayatafanyiwa kazi
  • Hatutapokea “testmonial”, “statement of results”, au “result slip” kwa Kidato cha Nne au Sita
  • Waombaji waliostaafu katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  • Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Recruitment Portal:
https://portal.ajira.go.tz
(Pitia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”)

Anwani ya Barua:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Songwe
S.L.P 77,
SONGWE

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19 Agosti, 2025.
Wahitimu wote wenye sifa wanahimizwa kutuma maombi kwa wakati.

Read also: