Nafasi za Kazi Wilaya ya Shinyanga

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na uwezo kujaza nafasi za kazi zilizoidhinishwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia kibali chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025.

Nafasi hizi ni za ajira ya kudumu kama ifuatavyo:

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

KadaIdadi ya NafasiSifa za MwombajiMajukumu MakuuNgazi ya Mshahara
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II4– Kidato cha IV au VI- Stashahada/NTA Level 6 katika Utunzaji wa Kumbukumbu- Ujuzi wa Kompyuta– Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka- Kusambaza na kurudisha majalada- Kutafuta kumbukumbu na kufuatilia mzunguko wa majaladaTGS C
Dereva Daraja la II10– Kidato cha IV- Leseni ya Daraja E au C yenye uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali- Cheti cha Mafunzo ya Udereva (VETA au kinachotambuliwa na Serikali)- Mafunzo ya Basic Driving Course– Kukagua gari kabla/baada ya safari- Kuwapeleka watumishi safari za kikazi- Matengenezo madogo ya gari- Kukusanya na kusambaza nyaraka- Kujaza logbook na kufanya usafi wa gariTGS B

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 (isipokuwa walioko kazini Serikalini).
  2. Kuwasilisha Detailed CV yenye anuani, namba za simu na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
  3. Kuambatanisha nakala za vyeti vya Elimu, Taaluma na cheti cha kuzaliwa.
    • Result slips, Provisional Results, Statement of Results na Transcripts hazitakubalika.
  4. Waombaji waliosoma nje ya nchi waambatishe uthibitisho wa NECTA (kwa Kidato cha IV/VI) au TCU (kwa elimu ya juu).
  5. Waombaji wenye mahitaji maalum waeleze katika maombi yao.
  6. Waombaji waliostaafishwa hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  7. Wasailiwa wenye majina yanayotofautiana kwenye vyeti watoe Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) kilichosajiliwa.
  8. Waombaji watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
  9. Mwisho wa kutuma maombi: 29/08/2025.

Jinsi ya Kutuma Maombi

  • Waombaji waandike barua ya maombi iliyosainiwa (kwa Kiswahili au Kiingereza) ikielekezwa kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
S.L.P. 113
Iselamagazi – Shinyanga

Kumbuka: Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafikiriwa.

Soma zaidi: