Table of Contents
Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi 11 za kazi baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Majukumu Makuu (2) | Sifa za Mwombaji | Ngazi ya Mshahara |
|---|---|---|---|---|
| Dereva II | 4 | • Kukagua gari kabla/baada ya safari.• Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi. | Kidato cha IV, leseni daraja C au E, uzoefu ≥ mwaka 1 bila ajali, cheti cha mafunzo ya msingi ya udereva (VETA/NIT au kinachotambuliwa na Serikali). | TGS B |
| Mwandishi Mwendesha Ofisi II | 3 | • Kuchapa barua na nyaraka za kawaida/siri.• Kupokea wageni na kushughulikia taarifa zao. | Kidato cha IV/VI, Stashahada (NTA level 6) ya Uhazili, ufaulu wa Hatimkato (Kiswahili & Kiingereza) maneno 100/dakika, mafunzo ya kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher). | TGS C |
| Msaidizi wa Kumbukumbu II | 4 | • Kuorodhesha barua zinazoingia/zinazotoka.• Kusambaza na kutunza majalada. | Kidato cha IV/VI, Stashahada (NTA level 6) ya Masjala/Utunzaji kumbukumbu, ujuzi wa kompyuta. | TGS C |
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18–45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba (waainishe aina ya ulemavu).
- Ambatanisha CV, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
- Waombaji waliomaliza nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA/NACTVET/TCU.
- Waombaji wa kada ya Dereva lazima waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Mwisho wa kutuma maombi: 01 Oktoba 2025.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Andika barua ya maombi iliyosainiwa na elekeza kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE,
S.L.P. 148, RUNGWE
- Tuma kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal): https://portal.ajira.go.tz
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments