Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega amepata kibali cha ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 (Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29.04.2025) kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kutokana na kibali hicho, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki ili kujaza nafasi za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Nafasi ya Kazi | Idadi ya Nafasi | Ngazi ya Mshahara | Sifa za Mwombaji |
---|---|---|---|
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II | 5 | TGS C | Kidato cha IV/VI, Stashahada ya Uhazili au NTA Level 6, ufaulu wa Hatimkato (Kiswahili & Kiingereza maneno 100/dakika), ujuzi wa kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher). |
Dereva Daraja la II | 6 | TGS B | Kidato cha Nne, leseni Daraja C au E, uzoefu angalau mwaka 1 bila ajali, cheti cha msingi cha udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali. |
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II | 2 | TGS C | Kidato cha IV/VI, Stashahada ya Utunzaji wa Kumbukumbu (NTA Level 6), ujuzi wa kompyuta. |
Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18–45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu wao.
- Waombaji waambatanishe CV yenye taarifa binafsi, mawasiliano, na majina ya wadhamini watatu.
- Waambatanishe nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria/wakili.
- Vyeti vya provisional results, statement of results, au results slip HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na NECTA, NACTVET au TCU.
- Waliostaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji wa kada ya dereva lazima waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Waajiriwa wa Serikali waliopo hawaruhusiwi kuomba.
- Taarifa za kughushi hazitakubalika na zitachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi: 28 Agosti 2025.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal):
https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatazingatiwa.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments