Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu anatangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa kupitia kibali cha ajira mpya kilichotolewa na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Nafasi Zinazotangazwa
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II (Nafasi 4)
Majukumu:
- Kuchapa nyaraka (kawaida na siri)
- Kupokea na kuelekeza wageni
- Kutunza ratiba, kumbukumbu na miadi ya Mkuu wa Idara
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha IV au VI
- Diploma ya Uhazili au NTA Level 6 ya Uhazili
Mshahara: TGS C1
2. Dereva Daraja II (Nafasi 5)
Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari
- Kuwasafirisha watumishi
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha IV au VI
- Leseni ya Daraja E au C
Mshahara: TGS B1
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18–45
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na wataje aina ya ulemavu
- Ambatanisha CV, namba za simu, barua pepe, majina ya wadhamini 3
- Ambatanishe vyeti halisi vilivyothibitishwa na wakili:
- Cheti cha Form IV/VI
- Cheti cha mafunzo ya taaluma
- Vyeti vya Kompyuta
Mwisho wa Kutuma Maombi
Tarehe ya mwisho: 14/08/2025
Anuani ya Barua ya Maombi:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu,
S.L.P 246,
Nanyumbu – Mtwara.
Tuma maombi kupitia mfumo wa ajira:
https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu HAYATAFIKIRIWA.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments