Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu anawaalika Watanzania wenye sifa kuomba ajira mpya na mbadala zilizopatikana kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 kupitia vibali rasmi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Nafasi Zinazotangazwa
1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II – Nafasi 12
Majukumu:
- Kuchapa barua na nyaraka (za kawaida na za siri)
- Kupokea wageni na kuwaelekeza
- Kutunza kumbukumbu za ratiba, vikao, safari
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha IV au VI
- Stashahada ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6
Mshahara: TGS C
2. Dereva Daraja II – Nafasi 3
Majukumu:
- Kukagua gari kabla/baada ya safari
- Kuwasafirisha watumishi kikazi
Sifa za Mwombaji:
- Kidato cha IV na cheti cha mtihani
- Leseni ya Daraja “E” au “C”
Mshahara: TGS B
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Raia wa Tanzania, umri miaka 18 hadi 45
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja aina ya ulemavu
- Waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na wakili
- Waajiriwa wa umma kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba
- Ambatishe CV, namba za simu na wadhamini 3
- Vyeti vya taaluma (Kidato cha IV, VI, taaluma husika) vithibitishwe na wakili
Tarehe ya Mwisho na Namna ya Kutuma Maombi
Mwisho wa kutuma maombi: 14/08/2025
Anuani ya Barua:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,
S.L.P 97,
Kasulu.
Tuma Maombi Kupitia:
https://portal.ajira.go.tz
Maombi yasiyowasilishwa kwa njia hii hayatapokelewa.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments