Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, kupitia kibali kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujaza nafasi mbalimbali kama ifuatavyo:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 4
Sifa:
- Elimu ya kidato cha Nne au Sita
- Stashahada (Diploma – NTA Level 6) ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
- Uwezo wa kutumia kompyuta
Majukumu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka
- Kusambaza na kurudisha majalada
- Kufuatilia mzunguko wa majalada katika ofisi
Mshahara: TGS C
2. Dereva Daraja la II – Nafasi 3
Sifa:
- Cheti cha Kidato cha Nne
- Leseni ya daraja E au C, na uzoefu wa angalau mwaka 1 bila kusababisha ajali
- Vyeti vya mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambulika na Serikali
Majukumu:
- Kukagua gari kabla/baada ya safari
- Kuwapeleka watumishi katika safari za kikazi
- Matengenezo madogo madogo na kutunza “logbook”
- Kusambaza nyaraka na kufanya usafi wa gari
Mshahara: TGS B
Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
- Umri miaka 18 – 45
- Raia wa Tanzania
- Vyeti vya elimu na taaluma viwe vimehakikiwa na kuidhinishwa na mwanasheria/wakili
- Testimonials, Statement of Results, au Provisional Results hazitakubalika
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi
- Vyeti vya nje ya Tanzania viwe vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTVET
- Waombaji waliostaafu au walioko tayari kazini Serikalini hawapaswi kuomba (isipokuwa kwa kibali maalum)
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatume kupitia mfumo wa ajira wa Serikali:
https://portal.ajira.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi: 14 Agosti, 2025
Anuani ya barua ya maombi:
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua,
S.L.P 83
KALIUA
Maombi yasiyotumwa kwa mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments