Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025. Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 05
Majukumu:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari
- Kuwapeleka watumishi safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo ya gari
Sifa:
- Cheti cha Kidato cha Nne
- Leseni ya Daraja E au C
- Uzoefu wa mwaka 1 bila kusababisha ajali
- Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali
Mshahara: TGS B1
2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 04
Majukumu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka
- Kusambaza majalada kwa watendaji
Sifa:
- Kidato cha Nne au Sita
- Diploma ya Utunzaji Kumbukumbu (NTA level 6)
- Ujuzi wa kompyuta
Mshahara: TGS C
3. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 05
Majukumu:
- Kuchapa nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea wageni na kuwaelekeza
Sifa:
- Kidato cha Nne/Sita
- Diploma ya Uhazili au NTA level 6 ya uandishi
- Hatimkato ya Kiswahili & Kiingereza (maneno 100 kwa dakika)
- Ujuzi wa programu za ofisi: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher
Mshahara: TGS C
Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri miaka 18 hadi 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi
- Ambatanisha CV yenye maelezo kamili, namba ya simu, email, na majina ya wadhamini 3
- Ambatanisha vyeti halisi vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili (Form IV, VI, Diploma n.k.)
- Statement of results au result slips hazikubaliki
- Aliyesoma nje ya nchi, vyeti viwe vimehakikiwa na NECTA/NACTVET/TCU
- Aliyestaafu utumishi wa umma haruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
- Vyeti vya mafunzo ya udereva ni lazima kwa waombaji wa nafasi ya dereva
- Usitumie taarifa za kughushi – hatua za kisheria zitachukuliwa
- Barua ya maombi lazima isainiwe na ielekezwe kwa:
Jinsi ya kutuma maombi
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Ajira:
https://portal.ajira.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi: 14 Agosti, 2025.
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
12 Njia Panda ya Mgama,
S.L.P. 108,
IRINGA.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments