Nafasi za Kazi Wilaya ya Arusha 2025

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za lazo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha 2025 anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira mpya baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Pendekezo kwa wanafunzi:

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

KadaIdadi ya NafasiSifa za MwombajiNgazi ya Mshahara
Dereva Daraja la II4– Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV). – Awe na Leseni ya Daraja E au C yenye uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali. – Awe amehitimu Mafunzo ya Msingi ya Udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambulika na Serikali.TGS B1
Dereva Mitambo 2S. L. P. 2330, 27 Barabara ya Halmashauri , 23382 Kiutu email: ded@arushadc.go.tz/tovuti: www.arushadc.go.tz 1.2.2 SIFA ZA KUAJIRIWA Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha nne ambao wana leseni Daraja la “G” ya kuendesha Mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitamboTGOS A
Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II2Mwombaji anatakiwa awe na Elimu ya kidato cha Nne Stashahada (NTA level 6 ) ya Uhazili (Secretarial Studies) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.TGS C

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Mwombaji awe Raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
  2. Aambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na wakili au mwanasheria.
  3. Awe na maelezo binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu, barua pepe, na wadhamini watatu.
  4. Aambatishe vyeti halisi vilivyothibitishwa vya taaluma na elimu.
  5. Matokeo (Result Slips), Testimonials, Statement of Results hazitakubaliwa.
  6. Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na TCU, NECTA au NACTE.
  7. Wastaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  8. Waajiriwa wa Serikali wasiombe kwa nafasi za kuingilia moja kwa moja.
  9. Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi na kuainisha aina ya ulemavu.
  10. Wenye majina tofauti kwenye vyeti wawasilishe Hati ya Kiapo (Deed Poll).
  11. Maombi yenye taarifa za kughushi yatatupiliwa mbali na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
  12. Waombaji wanaoitwa kwenye usaili wanashauriwa kuvaa mavazi yanayozuia baridi kwa kuzingatia hali ya hewa ya Arusha.

Namna ya Kutuma Maombi

  • Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Recruitment Portal: https://portal.ajira.go.tz
    (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”)
  • Barua za maombi ziandikwe kwa jina la:

MKURUGENZI MTENDAJI
S.L.P. 2330
23382 BARABARA YA HALMASHAURI
ARUSHA

Pakua PDF hapa.

Mwisho wa Kutuma Maombi

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14 Disemba, 2025.

Soma zaidi: