Table of Contents
Hili hapa tangazo la nafasi za lazo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira mpya baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Sifa za Mwombaji |
|---|---|---|
| Msaidizi Maendeleo ya Jamii | 7 | Kuajiriwa mwenye Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali |
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Waombaji wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa walioko Utumishi wa Umma).
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na waainishe aina ya ulemavu kwenye mfumo wa ajira.
- Maombi yaambatane na nakala za vyeti vya kuzaliwa, elimu (Form IV, VI, Diploma, Degree) vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Vyeti vya matokeo (Testimonials, Statement of Results, Provisional Results) havitakubalika.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE.
- Waombaji waliostaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Taarifa za kughushi zitaathiri moja kwa moja mchakato wa maombi.
- Maombi yasiyo katika utaratibu wa kielektroniki hayatafanyiwa kazi.
Namna ya Kutuma Maombi
- Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Recruitment Portal: https://portal.ajira.go.tz
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”) - Barua za maombi ziandikwe kwa jina la:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Busega,
22 Barabara ya Bomani,
S.L.P 157,
39582 BUSEGA – SIMIYU.
Mwisho wa Kutuma Maombi
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21 November, 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments