Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Ibara ya 113 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura 237 vinaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi wa Mahakama ya Tanzania wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi Mahakama ya Tanzania katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
| No. | Kada | Nafasi | Kituo cha Kazi |
|---|---|---|---|
| 1 | Mlinzi | Nafasi 101 | Mahakama ya Tanzania |
| 2 | Msaidizi wa Ofisi | Nafasi 88 | Mahakama ya Tanzania |
| 3 | Dereva II | Nafasi 63 | Mahakama ya Tanzania |
| 4 | Mpishi II | Nafasi 10 | Mahakama ya Tanzania |
| 5 | Afisa Ugavi Msaidizi I | Nafasi 18 | Mahakama ya Tanzania |
| 6 | Afisa Ugavi II | Nafasi 5 | Mahakama ya Tanzania |
| 7 | Mwandishi Mwendesha Ofisi II | Nafasi 63 | Mahakama ya Tanzania |
| 8 | Afisa Manunuzi II | Nafasi 10 | Mahakama ya Tanzania |
| 9 | Afisa Utumishi II | Nafasi 8 | Mahakama ya Tanzania |
| 10 | Operata wa Kompyuta II | Nafasi 6 | Mahakama ya Tanzania |
| 11 | Mhasibu II | Nafasi 6 | Mahakama ya Tanzania |
| 12 | Hakimu Mkazi II | Nafasi 52 | Mahakama ya Tanzania |
Ingia kwenye Mfumo wa Maombi ya Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania (JSC)
Maelezo Muhimu kwa Waombaji wa Kazi (Kada Zote)
- Uraia: Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania.
- Namna ya Kutuma Maombi:
- Maombi yatumwe kielektroniki pekee kupitia tovuti ya Tume: www.jsc.go.tz
- Nakala ngumu hazitapokelewa.
- Nyaraka za Kupakia (Upload):
- Barua ya maombi iliyosainiwa, ikielekezwa kwa:
Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama, S.L.P 2705, Dodoma. - Vyeti vya elimu, mafunzo na matokeo yake.
- Cheti cha kuzaliwa.
- Picha ya rangi (passport size) ya hivi karibuni.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Nyaraka nyingine kulingana na maelekezo ya fomu.
- Barua ya maombi iliyosainiwa, ikielekezwa kwa:
- Aina ya Ajira: Hizi ni ajira mpya; watumishi wenye ajira za kudumu serikalini hawaruhusiwi kuomba.
- Umri: Miaka 18–45, na asiwe amewahi kutiwa hatiani au kufungwa jela.
- Uwezo wa Kupangiwa Kituo: Watakaofaulu na kuajiriwa watapangiwa kwenye kituo chochote chenye nafasi ndani ya Mahakama ya Tanzania.
- Vyeti vya Nje ya Nchi: Lazima vithibitishwe na TCU/NACTE; bila hivyo maombi hayatazingatiwa.
- Waliofukuzwa/Kuachishwa Kazi: Hawaruhusiwi kuomba.
- Sifa na Masharti: Waombaji wasiokidhi vigezo au watakaopuuza masharti, maombi yao hayatashughulikiwa.
- Taarifa za Uongo: Kuwasilisha taarifa za uongo (mfano umri, elimu au uzoefu wa kazi) kutasababisha kufutwa kazini na kuchukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji Wenye Ulemavu: Watapewa kipaumbele; waeleze aina ya ulemavu katika barua ya maombi.
- Uzingatiaji wa Sifa: Mwombaji asiye na sifa za nafasi anayoomba au anayepuuza maelekezo haya, maombi yake hayatapokelewa.
- Mawasiliano ya Msaada:
- Simu: 0734 219 821 / 0738 247 341
- Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz
- Mwisho wa Kutuma Maombi: 29 Novemba 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments