Nafasi za Kazi Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha waombaji kazi wa Tanzania wenye sifa stahiki na uwezo wa kujituma kuomba nafasi (30) zilizotajwa hapa chini.

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC)

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ni chombo cha serikali chenye dhamana ya kusimamia masuala yote ya nishati ya atomiki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. TAEC ilianzishwa chini ya Sheria ya Nishati ya Atomiki Na. 7 ya 2003 (Cap 188) na ina jukumu la kudhibiti na kusimamia matumizi ya nishati ya atomiki na teknolojia ya nyuklia ili kulinda wafanyakazi, wagonjwa, umma na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi (Ionizing na Non-ionizing).

Pia, ina wajibu wa kuratibu na kuendeleza uhamishaji wa teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo ya taifa.

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

Na.Nafasi ya KaziIdadi ya Nafasi
1Radiation Safety Inspector II (Radiation Protection)4
2Research Assistant (Manufacturing Engineering)1
3Nuclear Instrumentation Technician II (Mining Engineering)1
4Nuclear Instrumentation Technician II (Biomedical Engineering)1
5Nuclear Instrumentation Technician II (Computer Engineering)1
6Nuclear Instrumentation Technician II (Electronics and Telecommunication Engineering)2
7Nuclear Instrumentation Technician II (Electrical Engineering)2
8Research Assistant (Industrial Engineering)1
9Research Assistant (Mining)1
10Research Assistant (Biomedical Engineering)1
11Research Officer II (Nuclear Science)1
12Research Officer II (Radiochemistry)1
13Research Officer II (Agriculture)1
14Research Officer II (Geology)1
15Assistant Radiation Safety Inspector II3
16Radiation Safety Inspector II (Nuclear Physics)4
17ICT Officer II (Programmer)1
18Receptionist II2
19Artisan II (Air Conditioning)1

Masharti ya Jumla ya Maombi:

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
  2. Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
  3. Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
  4. Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
  5. Haikubaliki kuambatanisha results slipstestimonials au partial transcripts.
  6. Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
  7. Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  8. Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  9. Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
  10. Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
  11. Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
  12. Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
  13. Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portalhttp://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).

Mwisho wa kupokea maombi: 24 Agosti 2025.

Soma zaidi: