Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Wakala wa Ufundi Umeme, Mashine na Elektroniki Tanzania (TEMESA), kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), inawaalika Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi zilizoainishwa hapa chini.
TEMESA ilianzishwa tarehe 26 Agosti 2005 chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Na. 30 ya mwaka 1997, ikiwa na jukumu la kutoa huduma bora na za haraka za umeme, mashine, elektroniki, usafirishaji kwa vivuko pamoja na upangishaji wa mitambo kwa taasisi za Serikali na umma.
Kwa sasa TEMESA ipo kwenye mchakato wa mageuzi makubwa ya kuongeza ushindani, ufanisi na kuridhisha wateja.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Cheo cha Kazi | Idadi ya Nafasi | Mwajiri | Masharti ya Kazi | Mshahara |
---|---|---|---|---|
Meneja wa Mkoa (Regional Manager) | 1 | TEMESA | Ajira ya Kudumu na Mafao ya Pensheni | TMSS 10 |
Meneja wa Huduma za Ushauri (Manager of Consultancy Services) | 1 | TEMESA | Ajira ya Kudumu na Mafao ya Pensheni | TMSS 10 |
Majukumu Makuu (kwa ufupi)
Meneja wa Mkoa:
- Kusimamia shughuli za kila siku za mkoa kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ubora na kwa wakati.
- Kusimamia rasilimali (vifaa, mitambo, nyenzo) bila gharama zisizohitajika.
- Kuandaa na kusimamia bajeti ya mkoa.
- Kuimarisha huduma kwa wateja na kupanua wigo wa kibiashara ndani ya mkoa.
- Kusimamia wafanyakazi, kuwajengea uwezo na kufanya tathmini za utendaji.
Meneja wa Huduma za Ushauri:
- Kusimamia na kuratibu miradi ya ushauri wa kitaalamu kutoka mwanzo hadi mwisho.
- Kutafuta na kuendeleza wateja wapya na kushirikiana na wadau mbalimbali.
- Kuhakikisha miradi inakamilika kwa ubora, ndani ya bajeti na kwa muda uliopangwa.
- Kutengeneza ripoti za maendeleo na utendaji wa miradi.
- Kuweka mikakati ya kukuza huduma za ushauri wa TEMESA.
Sifa za Waombaji
- Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili katika moja ya fani:
- Utawala wa Biashara (Finance/Marketing), Uchumi, Uchumi na Takwimu, Utawala wa Umma, Uhandisi wa Umeme, Mitambo, Elektroniki au Electromechanical.
- Kwa wahandisi: Lazima wawe wamesajiliwa na ERB kama Wahandisi wa Kitaaluma.
- Uzoefu wa angalau miaka 8 katika fani husika.
- Uwezo wa Uongozi, Mawasiliano, Ubunifu, Uadilifu na Uwezo wa Kibiashara.
- Umri: Usiozidi miaka 45, isipokuwa waajiriwa wa Umma ambao hawatakiwi kuzidi miaka 55.
Masharti ya Ziada
- Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania.
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba.
- Kuambatanisha:
- CV yenye mawasiliano sahihi,
- Vyeti vilivyothibitishwa (Elimu, Taaluma, Kuzaliwa),
- Vyeti vya usajili wa kitaalamu pale inapohitajika.
- Testimonials, Statement of Results, Result slips havitakubaliwa.
- Vyeti vya nje vihakikiwe na NECTA, NACTE au TCU kulingana na aina ya cheti.
- Waombaji waliostaafu Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
- Waombaji waandike barua ya maombi (kwa Kiswahili au Kiingereza) yenye sahihi.
Jinsi ya Kutuma Maombi
- Maombi yote yawasilishwe kupitia Recruitment Portal: https://portal.ajira.go.tz
- Barua ya maombi iandikwe kwa:
Secretary,
President’s Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Tambukareli- Dodoma.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05 Oktoba 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments