Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma (PSRS) kinawaalika Watanzania wenye nguvu, wenye shauku, na wenye sifa stahiki kujiunga na kazi kwenye ajira mpya 126 zilizopo hapa chini.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ni mamlaka ya serikali iliyoanzishwa kusimamia, kuendesha, kutunza, na kuendeleza viwanja vya ndege vya umma kwa mtindo wa usimamizi wenye mwelekeo wa kibiashara.
Ajira Mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya nafasi | Mwajiri |
|---|---|---|
| Engineer II – Civil | 3 | TAA |
| ICT Officer II – Network | 1 | TAA |
| Architect II | 1 | TAA |
| Airport Operation Officer II | 1 | TAA |
| Customer Service Officer II | 1 | TAA |
| Aircraft Marshaller II | 23 | TAA |
| Electrical Technician II | 2 | TAA |
| Mechanical Technician II | 2 | TAA |
| Assistant Airport Security Officer II | 74 | TAA |
| Artisans II – Plumbing | 12 | TAA |
| Artisans II – Civil | 2 | TAA |
| Artisans II – Mechanical | 1 | TAA |
| Artisans II – Electrical | 1 | TAA |
| Driver II | 2 | TAA |
Masharti Muhimu
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
- Aambatishe:
- Cheti cha kuzaliwa.
- CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
- Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
- Picha mbili (2) za rangi za passport size.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
- Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:
Secretary,
Presidents Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.
Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal): https://portal.ajira.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi: Tarehe 22 Novemba, 2025.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments