Nafasi za Kazi Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha waombaji kazi wa Tanzania wenye sifa stahiki na uwezo wa kujituma kuomba nafasi (52) zilizotajwa hapa chini.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tanzania Shipping Agencies Corporation, (TASAC) limeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania Sura ya 415 na kuanza kutekeleza majukumu yake rasmi kuanzia tarehe 23 Februari, 2018 kufuatia Tangazo la Serikali Na. 53 la tarehe 16 Februari, 2018.

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

NafasiIdadiMwajiriMwisho wa Kutuma Maombi
Boat Operator Daraja la II9TASAC22 Agosti 2025
Naval Architect Officer Daraja la II8TASAC22 Agosti 2025
Maritime Transport Officer Daraja la II15TASAC22 Agosti 2025
Flag and Port State Control Officer Daraja la II20TASAC22 Agosti 2025

Masharti ya Jumla ya Maombi:

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
  2. Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
  3. Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
  4. Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
  5. Haikubaliki kuambatanisha results slipstestimonials au partial transcripts.
  6. Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
  7. Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  8. Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  9. Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
  10. Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
  11. Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
  12. Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
  13. Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portalhttp://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).

Mwisho wa kupokea maombi: 22 Agosti 2025.

Soma zaidi: