Nafasi za Kazi Shirika la Posta Tanzania (TPC)

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Kwa niaba ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha waombaji kazi wa Tanzania wenye sifa stahiki na uwezo wa kujituma kuomba nafasi (46) zilizotajwa hapa chini.

Shirika la Posta Tanzania (TPC)

Shirika la Posta Tanzania (TPC) lilianzishwa kupitia Sheria ya Bunge Na. 19 ya mwaka 1993 na kuanza rasmi tarehe 1 Januari 1994 baada ya kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Mawasiliano la Tanzania (Tanzania Posts and Telecommunications Corporation) mwishoni mwa Desemba 1993.

TPC ni mtoa huduma pekee wa posta wa umma nchini, likiwa na jukumu la kutoa huduma za posta za bei nafuu, bora na zenye ufanisi kwa wananchi na maeneo yote nchini.

Shirika linafanya kazi zake chini ya mwongozo wa Sera ya Taifa ya Posta, Sheria za mashirika ya umma, masharti ya leseni iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na makubaliano ya Universal Postal Union (UPU) yaliyothibitishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo

NafasiIdadiMwajiriMwisho wa Kutuma Maombi
Postal Clerk7TPC22 Agosti 2025
Assistant Postal Officer II8TPC22 Agosti 2025
Public Relations Officer II1TPC22 Agosti 2025
Customer Service Officer II2TPC22 Agosti 2025
Postal Officer II8TPC22 Agosti 2025
Security Officer II2TPC22 Agosti 2025
Marketing Officer II (Business Development)2TPC22 Agosti 2025
Marketing Officer II (Sales)3TPC22 Agosti 2025
Marketing Officer II (Marketing)2TPC22 Agosti 2025
ICT Officer II (Security)1TPC22 Agosti 2025
ICT Officer II (Frontend Developer)1TPC22 Agosti 2025
ICT Officer II (Programmer – Mobile)2TPC22 Agosti 2025
ICT Officer II (Programmer – Backend)3TPC22 Agosti 2025
ICT Officer II (Network Administration)2TPC22 Agosti 2025
ICT Officer II (Database Administration)2TPC22 Agosti 2025

Masharti ya Jumla ya Maombi:

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
  2. Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao wazi kwenye mfumo wa maombi.
  3. Ambatanisha CV yenye taarifa sahihi za mawasiliano, anwani, barua pepe na simu.
  4. Maombi yaambatanishwe na nakala zilizohakikiwa za vyeti vya kitaaluma (Postgraduate, Shahada, Diploma, Cheti), matokeo ya kitaaluma, vyeti vya kidato cha IV na VI, vyeti vya usajili (kama inahitajika), na cheti cha kuzaliwa.
  5. Haikubaliki kuambatanisha results slipstestimonials au partial transcripts.
  6. Weka pasipoti-size picha ya hivi karibuni kwenye mfumo wa maombi.
  7. Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  8. Wastaafu wa utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba.
  9. Taja waamuzi watatu (referees) wenye mawasiliano sahihi.
  10. Vyeti vya shule vilivyotolewa nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vyeti vya kitaaluma vihakikiwe na TCU au NACTE.
  11. Barua ya maombi iwe na sahihi, iandikwe Kiswahili au Kiingereza
  12. Walioteuliwa tu ndio watajulishwa tarehe ya usaili.
  13. Nyaraka au taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yatumiwe kupitia Recruitment Portalhttp://portal.ajira.go.tz/ (pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS kwa kubofya Recruitment Portal).

Mwisho wa kupokea maombi: 22 Agosti 2025.

Soma zaidi: