Nafasi za Kazi SGR, TRC Kuajiri Wafanyakazi 2,460

Bonyeza KUJIUNGA NASI WHATSAPP Kwa nafasi za kazi, matangazo mbalimbali Ajira mpya kutoka Serikalini, Kampuni, Taasisi mbalimbali TAESA, Viwandani, Internships.

Nafasi za kzai Dar es Salaam, Agosti 20, 2025 – Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza mpango wa kuajiri wafanyakazi 2,460 kwa ajili ya mradi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kwenye vipande vya kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora, Dodoma.

Maelezo Muhimu

  • Utekelezaji wa ajira hizi umegawanywa kwa awamu:
    • Mwaka wa fedha 2024/2025, zaidi ya 500 tayari wameajiriwa.
    • Mwaka wa fedha 2025/2026, ajira 272 zitatolewa.
    • TRC itaendelea kuajiri hadi kufikia jumla ya 2,460.
  • Ajira hizi ni mbali na zaidi ya ajira 115,000 ambazo tayari zimetokana na makandarasi kwenye vipande vya ujenzi kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora (kipande cha kwanza hadi cha sita).

Mchanganuo wa Ajira 115,000 za Makandarasi

  • 35,000: Ajira za moja kwa moja.
  • 80,000+: Ajira zisizo za moja kwa moja, ikiwemo makundi kama:
    • Baba na mama lishe.
    • Wendesha bodaboda na bajaji.
    • Watoa huduma za mawasiliano (vocha, laini za simu n.k).

Umuhimu kwa Watanzania

Ajira hizi ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati, hususan SGR, inanufaisha wananchi, hasa vijana wanaoishi karibu na maeneo ya miradi pamoja na wenye ujuzi na elimu mbalimbali.

Mradi wa SGR umeendelea kuwa kichocheo cha ajira na ujuzi, ukiwa tayari umetengeneza zaidi ya 115,000 fursa za ajira kwa Watanzania katika sekta rasmi na zisizo rasmi.

Chanzo cha habari mwananchi

Soma zaidi: