Hili hapa tangazo la Ajira Mpya Mwalimu Daraja la III B Hisabati 1218 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 1218 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
| Kada | Idadi ya Nafasi | Ngazi ya Mshahara |
|---|---|---|
| Mwalimu Daraja la III C – Biolojia | 1218 | TGTS- D |
Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Baiolojia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Baiolojia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
Masharti Muhimu
- Awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18–45.
- Aambatishe:
- Cheti cha kuzaliwa.
- CV yenye taarifa binafsi na mawasiliano.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya uraia.
- Nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
- Picha mbili (2) za rangi za passport size.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi waambatishe vyeti vilivyothibitishwa na TCU/NACTE/NECTA.
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
- Taarifa za kughushi zitapelekea hatua za kisheria.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Barua za maombi (ikiandikwa kwa mkono) ziambatane na vyeti vyote muhimu na zitumwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Novemba, 2025 saa 9:30 Alasiri.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments