Hili hapa tangazo la nafasi za kazi 50 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Morogoro (MORUWASA) ni taasisi inayojitegemea chini ya Wizara ya Maji, iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019. Lengo lake ni kutoa huduma bora, endelevu na salama za maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro.
Ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake, MORUWASA inawatangazia Watanzania wenye sifa stahiki nafasi za ajira za mkataba wa mwaka mmoja (1) kama ifuatavyo:
Ajira mpya zilizotangazwa na Maelezo
Nafasi ya Kazi | Idadi ya Nafasi | Sifa za Mwombaji |
---|---|---|
Fundi Sanifu Msaidizi II (Artisan II) | 48 | – Awe amehitimu Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).- Awe na Cheti cha Ufundi Daraja la II/Level II katika fani ya Plumbing and Pipe Fitting.– Ujuzi wa kompyuta utapewa kipaumbele. |
Dereva Daraja la II (Driver II) | 2 | – Awe na Cheti cha Elimu ya Sekondari (Form IV au VI).- Awe na leseni halali ya udereva Daraja C au E, na mafunzo ya msingi ya udereva.- Awe na uzoefu wa angalau mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. |
Majukumu ya Msingi
Kwa Fundi Sanifu Msaidizi II:
- Kutambua na kuripoti uvujaji au upotevu wa maji.
- Kusoma mita za maji na kusambaza bili kwa wateja.
- Kufanya kazi za kuunganisha na kukata huduma za maji.
- Kukagua mita za maji na kuripoti miunganisho isiyo halali.
- Kusaidia ukusanyaji wa madeni na kuhifadhi taarifa katika mfumo wa wateja.
Kwa Dereva Daraja la II:
- Kuendesha magari ya MORUWASA kwa kufuata sheria za barabarani.
- Kukagua magari kabla na baada ya safari na kutoa taarifa za hali ya gari.
- Kuhakikisha gari linakuwa safi na salama muda wote.
- Kufanya matengenezo madogo ya gari na kuripoti kasoro.
- Kusafirisha nyaraka, barua na mizigo ya taasisi.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Barua ya maombi iambatane na Wasifu binafsi (CV) unaoonyesha majina, anuani, barua pepe na namba ya simu.
- Waambatanishe nakala halisi zilizothibitishwa za vyeti vya elimu.
- Vyeti vya matokeo (Form IV/V/VI Results Slips) na Testimonials havitakubaliwa.
- Ambatanisha picha moja ya pasipoti (passport size) na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
- Watu wenye mahitaji maalum wanahimizwa kuomba.
- Waombaji watakaowasilisha nyaraka za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Ni waombaji waliofanikiwa pekee watakaopigiwa simu kwa hatua zinazofuata.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yatumiwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo:
Managing Director,
Morogoro Water Supply and Sanitation Authority (MORUWASA),
S.L.P. 5476,
MOROGORO.
Mwisho wa Kutuma Maombi:
Ndani ya siku kumi na nne (14) tangu tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili.
Soma zaidi:
Leave a Reply
View Comments